Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Waluguru wanamsemo wao unaosema’Kigira Mwali Kifika’ Yaani siku ya kumnema Mwali imefika.
Keshokutwa jumapili ya April 16 nchi itasimama kwa dakika 90 kupisha Dabi ya Simba na Yanga iliyopangwa kupigwa siku hiyo majira ya saa 11 jioni Uwanja wa Mkapa ulipo Kata ya Mgulani Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam.
Timu hizo kubwa nchi zenye umri wa Zaidi ya Miaka 80 zinahistoria kubwa zinapokutana lakini hitori kubwa ambayo mpaka sasa inashikiriwa na Simba ni ya Mwaka 1977 ambapo Simba aliichapa Yanga bao 6-0.
Rekodi zinaonyesha Yanga haijawahi kulipa kisasi hicho cha kuifunga Simba bao 6 ingawa Yanga imeshaifunga Simba mara nyingine lakini si kwa idadi hiyo ya bao 6.
Katika gemu hiyo iliyopigwa Julai 19 1977 Mwiba mchungu alikuwa mchezaji wa Simba Abdallah ‘King’Kibadeni pekee alifunga mabao 3’Hat Trick’ huku Jumanne Hassan Masumenti akifunga bao 2 na bao la 6 Yanga walijifunga wenyewe kupitia kwa beki wao Seleman Said Sanga baada ya kupelekea Moto mkali na washambuliaji wa Simba.
Kufuatia hali hiyo siku za nyuma Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kufanya mahojiano Maalumu na Kibadeni ambaye alifunguka mazito juu ya tukio hilo la kuwachapa Yanga bao 6-0.
Stori hiyo ilisharuka hewani kwenye Mtandao huu[Pichani Mwandishi wa Mtandao huu [kushoto] akimhoji Kibadeni.
Yanga ya Msimu huu ni ya Moto kweli kweli ikiongoza ligi kwa muda mrefu ikiwa na Point 68 huku Simba akishika nafasi ya pili ikiwa na Point 60.
Kwa hesabu zilivyo Yanga aliyobakiza michezo 5 inahitaji Point 5 tu atwae ubingwa Msimu huu.
Gemu za Yanga zilizobaki ni pamoja na Simba, Dodoma Jiji, Singida Big Stars, Mbeya City na Tanzania Prisons.
Kwa upande wa Mashabiki wa Simba wao wanadai Yanga Ubingwa wachukue lakini lazima wawafunge kutia doa ubingwa wao.
Swali Je? Yanga hii ya Msimu hiyo yenye moto Mkali itaweza kulipa kisasi hicho cha bao 6-0? .
Je Kweli simba wataweza kuwafunga Yanga kutia doa ubingwa wao? Mswali yote hayo yatajibiwa keshokutwa kwenye Dabi hiyo kubwa kabisa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza timu hizo zilizofuzu robo fainali ya michuano ya CAF zilitoka sale.
DUA.
“Hee Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na nchini endelea kunipa zawadi ya Uhai niweze kufika hiyo Jumapili”.
No comments:
Post a Comment