Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, April 10, 2023

TANZIA. MWANAMUZIKI NGULI WA MUZIKI WA DANSI NCHINI AMEFARIKI DUNIA JIONI YA LEO.


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Baada ya kusingiziwa kifo mara kadhaa, hatimaye Mwanamuziki Mkongwe nchini mwenye sauti ya tausi Hussein Suleiman Jumbe amefariki dunia jioni ya leo katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.

 .

 Marehemu Jumbe 'Mtumishi'  enzi za uhai wake amezitumikia band kubwa za jijini Dar es salaam kabla ya miaka ya 2005 .kuhamia Mkoani Morogoro na kujiunga na band ya Mikumi Sound ‘Wana Tekenya’ inayoongozwa na ‘Mgosi’ Josse Kigenda.

Band hiyo  inatamba na kibao chake kisicho chuja kama tui la Nazi cha ‘Mama Mkwe Kisa gani’.

 

Nakumbuka  baada ya Jumbe kujiunga na Mikumi Sound alitunga wimbo wa Ua Jekundu unaopendwa na wengi japo Jumbe alihama band hiyo na kureja band za Dar lakini mpaka sasa band hiyo ya Mikumi yenye hati miliki ya Wimbo huo inaupiga kila siku huku Kigenda akiimba wimbo huo kwa kuiga sauti ya Jumbe.

 

Nakumbuka Jumbe baada ya kujiunga na Mikumi walianzisha upinzani wa Jadi na band ya Levent  Musca iliyokuwa ikimilikiwa na Meneja wa TANROARD  Mkoa wa Morogoro  Mhandisi Charles Madinda ambaye naye ametutangulia mbele za haki miaka kadhaa iliyopita.

 

Baadhi ya wanamuziki waliounda band hiyo ya Levent  ni pamoja na Mkongomani Pitchuu Kongo, Sad Bongisa ambaye kwa sasa anaishi nchini Spain, Fred Simkoko Mtoto wa kocha  Mkuu wa lhefu John Simkoko, Monica Kibena, Abdul White na Killer Boy ambaye kwa sasa ni mmiliki wa Band ya Waluguru Original.

 

Kuna siku band hizo zilizokuwa na upinzani mkali  kama ule wa Simba na Yanga zilipambanishwa Jukwaa Moja kwenye ukumbi wa CCM Mji Mkuu kumsaka mbambe wa Mji Kasoro bahari.

 

Kwenye shoo hiyo iliyohudhuliwa pia na Mwandishi wa Mtandao huu Huseni Jumbe alifunika na kibao chake hicho cha Ua Jekundum huku Levent  wakifunika kwenye shoo zilioongozwa na wanenguaji Amina Rusha Roho, Chiku na Bomoa.

 

“Inna Lillah Wainna lllah Najiun”.

 

“Tangulia kamanda Jumbe tutaonana baadae”.

“Sisi tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi tunamuomba akusamehe makosa yako na akuweke unapostahili Wote tuseme Amen.”

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...