Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, March 5, 2023

UJUMBE WA NENO LA MUNGU


 

1PETRO 3.3-7

Kujipamba kwenu kusije kujipamba kwa nje. Yaani kusuka nywele na kujitia dhahabu.na kuvalia mavazi.

 

Bali kuwe utu  wa moyoni usioonekana katika mapambo yasiyoharibika, yaani roho ya upole na utulivu iliyo ya thamani kuu mbele ya Mungu.

 

 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani waliomtumaini Mungu na kuwatii waume zao.

 

Kama vile sara alivyomtii lbrahimu.akamwita Bwana nanyi ni watoto wake  mfanyapo mema wala hamkutishwa kwa hofu yoyote.

 

Kadhalika nyinyi waume kaeni na wake zenu  kwa akili  na kumpa mke heshima  kama chombo kisicho na nguvu na kama warithi pamoja na neema ya uzima  kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

 

Hilo ndilo neno letu la leo Jumapili ya March 5.

 

Neno hili limejitosheleza sina cha kuchambua.lakini niulize swali moja tu kwamba kama Mungu anakemea wanawake kujipamba je kwa zamani hizi kwa wale wanaume wanaojipodoa kwa kujichubua na kusuka hukumu yao itakuwa je.?

 

 Yesu Kristo [Nabii lssa] anagonga hodi kwenye moyo wako mfungulie aingie

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...