Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, March 6, 2023

MTAMBO MAALUMU WA KUTENGENEZA POMBE YA KIENYEJI.



 

 

Nyumbani ni nyumbani. najivunia kuwa Msambaa hii ni  nilipowatembelea kwetu Tarafa ya Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.

 Jimbo la Mlalo linaongozwa na Mbunge wetu bora kabisa Mh Shangazi.

 

 lfahamishe sio shangazi yangu ni jina halisi la Mbunge  huyo mchapa kazi

Pichani Mkude Simba Kulia nikigonga Muwa huku machalii  kutoka Arusha wakigonga kikombe cha pombe  ya muwa maarufu pombe ya boha.

 

 Tunaumwagilia moyo kwenye baa ya Mmanyai iliyopo juu ya Milima ya Usambara eneo la Utondoro Mlalo Lushoto.

 

Chupa moja ya Pombe hiyo ni shilingi mia 5 kwa walevi ukigonga chupa tatu pekee unapata stimu ile ile kama umegonga Smath Gyn

Kwa batari mbaya au nzuri toka nitue hapa chini ya juwa sijawahi kunywa kilevi aina yoyote,

wakati washikaji zangu kutoka Arusha wakigonga kikombe cha Boha mimi niligonga Muwa halisi unaotengeneza Pombe hiyo ambayo ikishakamuliwa na mashine  huvundikwa kwa siku mbili kama ile pombe ya Mbege ya watani zangu Wachaga wa kule kijijini Uhuru Kishumundu.

 

Pichani Kulia machalii hao wakisukuma matambo wa kukamua miwa ambapo mwisho wa siku maji hayo ya muwa ugeuka kilevi.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...