Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, March 13, 2023

TUNAENDELEA KUHIMIZA AMANI KWENYE MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA






 

 KUMBUKIZI.

 

Mtandao huu Umefurahi Mikutano ya Vyama vya siasa kuruhusiwa baada ya kuzuiwa kwa  takribani miaka 6.

 

Pia Mtandao huu unaungana na wote wanahimiza Mikutano hiyo iwe ya kistaarabu kuziwepo na Vulugu wala maneno makali ya kuwaumiza wengine.

 

Aidha Mtandao huu unaamini hoja nzuri ndizo ambazo zitamvutia Mwananchi kuchangua mgombea yoyote atakayevutiwa na sera zake.

 

 CAPTION 

Pichani kulia
Mawaziri Wakuu Wastaafu waliokihama chama cha mapinduzi na kutimkia UKAWA  Mh Fredrick Sumaye[kushoto] na Mh Edward Lowassa ambaye kwenye uchanguzi mkuu wa mwaka 2015 alikuwa mgombea Urais kwa leseni ya Ukawa.

Mawaziri hao wakuu walinaswa na Mwandishi wa Mtandao huu wakisoma gazeti la Mwananchi kwenye mkutano wa kampeni wa Ukawa uliofanyika 2015 kwenye viwanja wa shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

 

 Kwa sasa Mawazi hao wakuu wamerejea kwenye chama chao cha CCM

 

Picha no 2 Rais Mstaafu wa awamu ya 4 Mh Jakaya Kikwete [Kulia] akiteta jambo na Katibu Mkuu  Mstaafu wa CCM Mh Yusuf Makamba kwenye mkutano wa kampeni ya kumnadi aliyekuwa mgombea Urais wa Chama hicho Hayati John Pombe Magufuli  mwaka 2015  Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

 

Picha no 3 Mwandishi wa Mtandao huu akipiga kura kwenye kituo cha Kata ya Mazimbu Jimbo la Morogoro kwenye uchanguo huo mkuu wa mwaka 2015.

                      MATOKEO

Nafasi ya Urasi alishinda Mgombea wa CCM Hayati Magufuli, Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini alishinda pia mgombea wa CCM Mh Aziz Abood na Udiwani wa Kata hiyo ya Mazimbu aliibuka kidedea Mgombea wa CCM Mh Pascal Kihanga ambaye kwa sasa ndiye Meya wa Manispaa ya Morogoro.

 

Picha zote na Maktaba ya Mtandao wa Shekidele.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...