Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, March 12, 2023

UJUMBE WA NENO LA MUNGU MALI ZAKO UNAKULA NA NANI?








 

MARKO 10 .41-45

 

“Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia  Yakobo na Yohana.

 

Yesu akawaita,akawaambia.mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa mataifa huwatawara kwa nguvu na wakubwa wao huwatumikisha.

 

Lakini haitakuwa hivyo kwenu,bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu,atakuwa mtumishi wenu.

 

Na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu,atakuwa mtumwa wa wote.

 

 Kwa maana mwana wa Adam naye hakuja kutumikiwa,bali kutumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”.

 

Hilo ndilo neno letu la leo Jumapili ya March 12. UCHAMBUZI. Mwana wa Shekidele naye hakuja duniani kujilimbikia mali bali kidogo alichajaliwa aliganawa na watu wenye uhitaji.

 

Pichani Mwana huyo wa Shekidele alitumia taaluma yake ya Uandishi wa habari na kufanikiwa kumjenga nyumba Mlemavu Mohamed Matama kupitia wadau mbali mbali wa pande zote za dunia.

 

Picha no 2 Mwana huyo wa shekidele akakabidhi mifuno ya Unga Sembe kwa kituo cha Watoto yatima cha Mkitunda kilichopo Kihonda Manispaa ya Morogoro. Picha no 3 Mwana huyo wa Shekidele akimkabidhi Pampu Muuguzi wa wodi ya watoto ambapo mtoto huyo jina linahifadhiwa mwenye umemavu alifichwa hcini ya kinda kwa muda wa miaka kadhaa na Mama yake Mzazi aliyekuwa akiishi Dumila Wilaya ya Kilosa.

 

Mwana huyo wa Shekidele baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema alitina Dumia na kumuibua Mtoto huyo chini ya Uvungu wa kitanda cha kamba.

 

 Picha no 4 Mwana huyo Shekidele akimkabidhi Pesa Mlemavu Jeremia Msafiri ambapo baada ya taarifa za Mlemavu huyo kutoka kwenye gazeti wadau mbali mbali kutoka mikoa yote ya Tanzania waliguswa na kutuma Pesa kiasi cha laki 6.

 

Baada ya kukusa pesa hizo zilizotumwa kwenye simu ya Mwana wa Shekidele alitoa na kumkabidhi Mlemavu huyo.

 

Kulia Mke wa Mlemavu huyo akimshukuru Mungu na msaada huo uliotolewa na taifa la watu wa Mungu wanaojali shida za wengine.

 

Somo hili linakukumbusha na kunikumbuksa mimi kwamba mali tulizonazo au madaraka tuliyo nayo yamwe msaada kwa wenzetu wenye uhitajiri tusijilimbikizie mali tukazila sisi na familia zetu pekee mali hizo ziwe nyingi au ndogo tugawana na wenzetu wenye uhitaji.

 

Binafsi najivunia kutumia kazi yangu ya Uandishi wa habari kufanikisha kumjengea nyumba ndugu yetu Matama.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...