Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, March 21, 2023

TASWIRA TAJIRI ABOOD KUKETI KWENYE MCHANGA



 

PICHA KALI YA WIKI.

 

 Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Dr Abdullaziz Mohamed Abood. Almaarufu Aziz Abood au Mtetezi wawanyonge akiketi chini ya mchanga akiwasikiliza kwa makini makada wenzake wa Chama Cha Mapinduzi’CCM’wa Jimbo la Morogoro.

 

Mh Abood ambaye pia ni Miongoni mwa Matajiri wakubwa nchini akimiliki, Viwanda, Mabasi, Malori, Vituo vya Mafuta na Vyombo vya habari Mali zake hizo nyingi ziko mkoani Morogoro.

 

Licha ya uataji huo mkubwa alionao na madaraka makubwa akiyonayo ya Ubunge wa Jimbo la Morogoro na MNEC wa CCM kamwe Mh Dr Abood sio mtu wa kilinga kujisikioa wala kuwadharau watu wasio na kipata. Tajiri Abood anayetajwa kuwa tajiri namba moja Mkoa wa Morogoro akifika kwenye msiba akikuta watu wanakula Ugari na Maharage naye anakula huo huo, akikuta watu hawana viti wanafanya mkutano wake huku wameketi chini ya Mchanga naye anaketi kwenye mchanga kama anavyoonekana Pichani.

 

Kama hiyo haitosho sisi tuliobahatika kuingia kwenye gereji yake tulishuhudia amagari mengi ya kifahari kama Jeep, Benz, Toyota V8[Mashangingi] lakini Mbunge huyo mara nyingi akiwa kwenye jimbo lake la Morogoro anatembelea gari la kawaida kabisa Toyota Previs rangi ya karoti.

 

Hii inadhihirisha kwamba hataika kuonekana wa dhamani kuliko wengine, vile vile Mh Abood amekuwa msaada mkubwa kwa wtu mbali mbali hasa wenye uhitajiri, Miongoni mwa vitu anavyosaidiua jamii ni kutoka mabasi yake kwenye Misiba ambapo mtu yoyote anayepatwa na msiba anapewa basi.

 Hivi karibuni  Abood ilimtunuku heshima ya U-daktari na Moja ya Chuo Kikuu cha Marekani ‘Academy Of Universal Global Peace’ baada ya kufanya utafiti na kubaini Mh Abood amekuwa kinara wa kusaidi Jamii.

 

Hafra hiyo ilifanyika jijini Dar es salaam na Pichani Mh Abood akiwa na cheti baada ya kununukiwa U-daktari huo wa heshima, binafsi ninavyomfahamu Mh Abood amestahiri kupokea heshima hiyo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...