Wana kwaya wa Kwaya ya Paradiso ya usharika huo Mchaga Jaccline[kushoto] na Msambaa Betha wakipozi mbele ya kamera za Mtandao huu. lfahamike Mwandishi wa Mtandao huu pia ni Mwana kwaya ya Kwaya hiyo ya Paradiso
Palishi weka wa Usharika huo [wa Kati] akishirikiana na wanawake wengine kuongoza lbada iliyofanyika juzi jumapili
Mwinyiristi wa Usharika huo Peter Nyange[mwenye kaunda suti] akifuatilia lbada hiyo iliyoongozwa na wanawake wa usharika huo
Kiongozi wa kina mama wa usharika wa Mji Mpya Jannete Mushi akimkabidhi Risara Mchungaji Dunia
Mmoja wakina mama hao akitoa mahubiri juu ya Membari walioinunua, chini ni uzi wa chuna wenye urembo ambao pia umenunuliwa na kina mama hao
Kwaya ya kina mama ikiendelea kuimba
...Wakipiga Picha ya pamoja na Viongozi wa kanisa hilo
Hili ndilo gari ambalo wamenunua wanawake wa Ushariki wa Mji Mpya
Wanawake hao wakiwa kwenye gari hilo
Gari hilo likiwa nje yakanisa hilo
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
WAKATI Leo Jumatano Mach 8 wanawake wote duniani wanaadhimisha siku yao, Umoja wa wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania’KKKT’ Dayosisi ya Morogoro Usharika wa Mji Mpya wamefanikiwa kununua gari la kisasa na kumkabidhi kwenye uongozi wa Usharika huo Mama kwenye Dayosisi hiyo.
Kwa mujibu wa kanisani hilo Jumapili ya Machi 6 ndio ilikuwa kilele cha siku ya Mwanamke duniani ambapo lbada zote ziliongozwa na wanawake, huku kinamama wa usharika huo wakitumia siku hiyo pia kukabidhi gari hilo.
Mmoja wa Viongozi wa Umoja huo wa wanawake Bi Jannete Moshi akisoma risara kwenye lbada hiyo alisema gari hilo walilinunua Novemba Mwaka jana na kuwekwa wakfu na Askofu wa kanisani hilo Dayosisi ya Morogoro Jacob Ole Mameo.
Baada ya kusoma risara hiyo Jannete alimkabidhi Mchungaji kiongozi wa Usharika huo Mchungaji Dunia.
Kwa upande wake Mchungaji Dunia baada ya pokea Risara hiyo alisema.
” Wanawake wa Usharika huu tunawapongeza sana kwa juhuzi nzenu za kujitoa, awari mlitukabidhi hii Membali, baadae mkaweka huu uzio wa chumba hapa madhebahuni na sasa mmenunua gari mpya na kukabidhi kwenye usharika.
Kuhusu ombi letu la kuomba mmoja ya Frem za biashara tunazoendelea kuzijenga hapo nje ya kanisa ombi lenu nimelipokea na tutalifanyia kazi”alisema
Baada ya lbada hiyo kutamatika wanawake hao waliovalia sare walipiga Picha ya pamoja na Viongozi wa kanisani baadae wakapiga picha kwenye gari hilo.
No comments:
Post a Comment