Kigogo wa Polisi Hayati Neema Manase
Neema Samwel Juma Mrs Mlokozi akiwa na Mama yake Mzazi hayati Kete Abdallah
Tumain Dustan Shekidelekushoto] na Neema D Shekidele
Mama Mjengo
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Machi 8 kila Mwaka dunia inaadhimisha siku ya Mwanamke Dunia, hivyo kila mtu hapa duniani kwa siku ya leo uadhimisha siku hiyo kwa kumtangaza hadharani Mwanamke au wanawake anao wapenda na kuwakubali kwa moyo wake wote.
Wengine huwatangaza kwa kuonyesha upendo wao kwa Mama zao, dada zao, watoto wao ama wake au wapenzi wao.
Mwandishi wa Mtandao huu katika kuadhimisha siku hiyo kama alivyofanya miaka ya nyuma anaendelea kufahamisha
ulimwengu kwamba hapa chini ya jua wanawake anaowapenda kutoka kwenye sakafu ya Moyo wake ni Mama yake Mzazi Tumaini Samweli Juma ‘Mrs Shekidele’ ambaye ni Muuguzi Mstaafu wa hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Wa pili ni Mama yake Mdogo Neema Manase Kamanda Mstaafu wa kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Pwani, ambaye miaka michache iliyopita Mungu alimpenda zaidi na kumtwaa katika utukufu wake hivyo kupitia siku hii ya wanawake tunaendelea kumuomba mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake na amuweke sehemu salama.
Wa tatu ni Mama yake Mdogo Neema Mulokozi ambaye pia ni Muuguzi Mstaafu wa hospital ya Hushen Road iliyopo Mikocheni Jijini Dar.
Na bibi yangu Mpendwa hayati Kete Batimayo Abdallah aliyeaga dunia mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 103.
Bibi kete ndiye aliyewazaa mama zangu hao pamoja na mjomba David Samwel Juma
Wengine ni watoto wake wa kike Tumain Dustan Shekidele na Mdogo wake Neema D, Shekidele, Afande Neema umetutangulia mbele za haki lakini tunaendelea kulienzi jina lake ambalo nimemrisisha Mjukuu wako Neema Dustan Shekidele hata kabla hujaondoka hapa dunia.
……………………………………………….
No comments:
Post a Comment