Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, February 1, 2023

BONDIA MANDONGA AFUNGUKA MAZITO KUMILIKI GARI.


 


 

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 

Kutoka Mpiga debe Stend ya mabasi ya Mikoani ya Msamvu Morogoro hadi kumiliki gari za kifahari.

 

Huyo si Mwingine ni Star wa ngumi kwa sasa nchini Tanzania Karim Mandonga’Mtu Kazi’ ambaye baada ya kufanya vizuri ulingoni na nje ya ulingo akiwa kivutio kwa tambo zake sambamba na misemo yake ya shombo kwa wapinzani wake.

 

Juzi kati baada ya kumiliki gari hilo na kurejea nalo Mkoani Morogoro alipokutana na Mwandishi wa Mtandao huu aliyempongeza kwa kumiliki chombo hiyo Mandogo alipokea salam hizo huku akitoa majibu haya.

 

” Ni kweli Shekidele kwa sasa namiliki hili gari ambapo toka nizaliwe  ndio gari langu la kwanza kumiliki kwa umri wangu huu miaka yote nimetembea kwa miguu kwa hasira kwa sasa safari zangu zote natembea na gari kasoro safari zile za kwenda chooni  pekee ndio siendi na gari”alisema Mandonga na kumuacha Mwandishi wa Mtandao huu akiangua kicheko.

 

Baada ya kumtwanga Mpinzani wake nchini Kenya hivi karibuni, bondia Mandonga kipenzi cha wana Morogoro anatarajiwa kupanda tena ulingo Moshi Mkoani Kirimanjaro ambapo Promota Maarufu  nchini Tanzania Meja Seleman Semunyu amethibitisha hilo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...