Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, January 10, 2023

YARIYOJILI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI.   MNENGUAJI APARAMIA NGUZO MASHABIKI MIDOMO WAZI.

Huyu sio Fundi Speaker ni mnenguaji Queen Hiace akifanya yake kileleni




                         Husna Bongo naye akifanya yake
                Huyu aliyejikunja sio kambale ni Husna Bongo

 

 

        Na Mlala Nnje Dustan Shekidele,Morogoro.

 

KATIKA hali ya kubuni mbinu za uchezaji Mnenguaji nyota wa Band Pendwa ya Maisha Mapya’Wana Full Vipaji’ Grece John Tutu’Maarufu Queen Hiace gari la dawa’ a.k.a Mama Kichanga ameamua kuparamia nguzo.

 

 Tukio hilo lililoshuhudiwa Live bila Chenga na Mlala Nnje limetokea ljumaa iliyopita kwenye shoo ya band hiyo iliyofanyika ukumbi mmoja jina kapuni uliopo pande za Mazimbu Mkani hapa.

 

Baada ya menguaji huyo kuparamia juu ya nguzo hiyo iliyobeba Speaker na ‘Ku Eckt’ kama anatengeneza  Speaker hiyo huku akikata nyonga ikiwa ni moja ya Vionjo alivyowaonyesha mashabiki wake waliojazana kwenye ukumbi huo.

 

Kama hiyo haitoshi Mnenguaji huyo aliposhuka juu ya nguzo hiyo alipanda tena juu ya kichwa cha Mpiga picha wa Mtandao huu aliyekuwa amechutama chini akimfotoa mapicha menenguaji huyo akiwa  juu ya nguzo hiyo.

 

 Kama kawaida yake alipokuwa juu ya kichwa cha Mlala Nnje Queen Hiace aliendelea kumwaga Uno Feni na kusababisha umati mkubwa wawatu kupiga kelele za kumshangilia huku baadhi yao wakisogea eneo la tukio na kummwagia mapesa Mnenguaji huyo.

 

Baada ya kushuka kwenye kichwa hicho Mnenguaji huyo alizoa mapesa aliyomwagiwa chini na kutimka zake bila kutoa fungu la 10 kwa Mlala Nnje aliyefanya naye korabo ya lazima.

 

Mnenguaji huyo alichoacha kwenye kichwa cha Mlala Nnje ni Jasho lake lililommwagika kama Mvua za Al-Nino kufuatia kazi kubwa aliyoifanya ya kuutikisa mwili wake.

 

Wengi walitamani kuona Picha ya tukio hilo  kwa bahati mbaya haikupatikana kwa sababu ya mazingira kuwa si rafiki kwani  kila Mlala Nje alipojaribu kupiga Picha hiyo akiwa chini huku mwili wake ikitikishwa kama kapigwa short ya Umeme aliambulia kunasa Paa la nyumba  hiyo huku Picha hiyo ikiwa ime sheck kwa mtikisiko uliosababishwa na mnenguaji huyo.

 

Kwenye shoo za band hiyo kuna kipengere cha wanenguaji  kuangushiwa Sebene Kavu kila mmoja kuonyesha umahiri wake kwa kucheza mmoja mmoja.

 

Hivyo baada ya Queen Hiace kushuka Jukwaani aliingi Husna Ramadhan Maarufu Husna Bongo ambaye naye alikinukisha ile ile kiasia cha kurembua Macho kama mtu aliyetafuna kungu au Milungi.

 


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...