kwa sasa serikali ya Mkoa imepiga Marufuku watu kwenda kula raha kwenye Bwawa hilo
Mastaa wa Moro Bondi Cheka Kushoto na Afande Sele wakipozi mbele ya Kamera za Mtandao huu
Shabiki Maarufu wa Tanzania Kutoka Morogoro hayati Ya Mungu
Bingwa wa Disco Afrika Mashariki na Kati Mwana Morogoro Super Ngedere
Na Dunstan Shekidele,Morogoro_
Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma
kidogo ya miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni...
Hii town ya wajanja , vijana wanaojua kuvaa,wenye
exposure, wapenda burudani na utafutaji...
Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na
upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa...
Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill iliyokua ikimilikiwa na Wahindi’Watanzania wenye Asili ya lndia na
Kigurunyembe inayomilikiwa na Kanisani Katoliki Jimbo la Morogoro,ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa Kishua madent wengi walikuwa ni wahindi na Waarabu
na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto
wa kitaa wengi wao wanatoka kwenye familia za maisha ya kawaida na Kati...
Kwa sasa shule hizo bado zipo lakini zimepoteza ule umaarufu baada ya zule nyingi binafsi kuanzishwa mkoani hapa.
lfahamikwa kwa sasa Neema Dustan Shekidele anasoma kidato cha 3 shule ya Sekondari Kigurunyembe
Mitaa maarufu ya kishua ni
Forest, Liti, SUA na Rock Garden...
Mitaa maarufu
ya Uswahirini ambako huko ukabaji ulikuwa nje nje ma laana zote ziko huko kama Vile Vigodoro na nyumba za matope na Vilabu vya Pombe za kienyeji ni Mji Mpya, Chamwino,Vibandani Kichangani, Msamvu na
Mafiga.
Watu wa Moro ni wapenzi sana wa burudani
haswa muziki na soka.... Kulikuwa na timu ya mji
maarufu Reli kiboko ya vigogo hii ilikuwa daraja
la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki..
Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, Deo Njohole,
David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono Peter Mjata, Juma Salum Msawila na Makipa Sahau Kambi na Athuman Msumari
hapo kuna mshangiliaji maarufu sana Hayati
Ya Mungu[Pichani aliyejichora] ambae ndio shabiki wa kwanza
mtanzania kujichora mwilini...
Licha ya Reli
mtaani kulikuwa na team nyingi sana za
mchangani kama Jamaica, Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae
ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso,
Rhino.
.
Kwenye muziki Moro ina historia ndefu
siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka
Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo
enzi za shimoni Morogoro Hotel na Rock Garden
na maonyesho ya Forest Hill... Hapa kuna mtu
anaitwa Dj Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa
Konga ndiye aliyemfundisha Udijei Dj Maarufu kwa sasa hapa nchini John Dilinga.
Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi
alikuwa anakuja Dj Joseph Kusaga akimfundisha
kazi Dj Peter Moe.
Miaka hiyo ya 90 Maneno Mohamed Ngedere Maarufu Super NgederelPichani anayecheza] alitwaa ubingwa wa Disco Mkoa wa Morogoro akiwabwaga wapinza wake wakubwa Bob Tiger Rhumba Boy na Askofu.
Baada ya kutwa ubingwa uliompa tiketi ya kushiriki mashindano ya Taifa.
Super Ngedere alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania akiwabwaga Madenza maarufu wa Dar es salaam kama vile Black Moses na Athuman Diga Diga.
Ubingwa huo pia ulimpa tiketi ya kushiriki mashinda ya Disco ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo huko Mluguru huyo kutoka Mji Mpya Morogoro alifanikiwa kutwaa ubigwa huo wa Afrika Mshariki na Kati akimbwana Mkenya Kanda Kids. Hadi Sasa Super Ngedere anaushikiria Ubingwa huo.
Moro ya Vipaji Mwaka 2003 Mwana Morogoro Mwisho Mwampamba alifanikiwa kushika nafasi ya pili ya mashindano ya Big Brother Afrika kwenye jumbe la South Afrika akinyakua zawadi ya Dora sawa na milion 50 za kibongo.
Wakati hiyo ya Mwisho haijapoa Mwaka 2004 Mwanamuziki Seleman Msindi ‘Afande Sele’ akifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkali wa Mashairi nchini ‘Mkali wa Rhymes’ na kumbuka siku hiyo mimi na Afande Sele tulikwenda kwa Mh Aziz Abood akatupa basi moja lililobeba mashabiki kuwapeleka ukumbi wa Diamond Jubilee Dar ilipofanyika fainari hiyo ya Mkali wa mistari nchini.
Tukagawana majukumu Afande Sele alitangulia Dar na gari lake na Mimi niliongoza kundi la mashabiki hao kuelekea Dar.
Nakumbuka majira ya saa 9 usiku kwenye ukumbi huo Wimbo wa Darubini Kali wa Afande Sele alitoka kuzifunika nyimbo zote za mastaa wa Dar kama vile kundi la TMK la Mkubwa Fera, Hoseph Haule’Prof J’. Joseph Mbilinyi’Sugu’ Mr Nice Madojo na Domo Kaya kutoka Arusha na Dudu Baya.
Mwandaaji wa mashindano hayo Eric Shigogo alimkabidhi zawadi ya gari Jipya Afande Sele ambaye mpaka sasa anashikilia ubingwa huo wa Mkali wa Vina Tanzania.
Tukasogea mbele kidogo miaka ya 2017 hivi Bondia Francis Cheka[Pichani akiwa na Afande Sele] aliwachapa mabondia wote wa Tanzania ikiwemo familia yote ya Matumla ambayo aliipiga kama Ngoma.
Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe.. Kulikuwa na watemi wa mji kama vile Slim, Daso, Mzee Kisaka, Matata, Gamba mcheza judo, na vijana wa
siafu toka mji mpya.
Tunaposema Moro inakila kitu tunamaanisha kwa ushahidi kwenye mbio za magari pia Moro ilikuwa tishio.
Wakimbiaji wa magari maarufu kina
Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos hawa jamaa waliuwakilisha vyema Mkoa wa Morogoro kwenye mbio za magari zilizofanyika popote Tanzania.
Kwenye mazuri pia kuna mabaya miaka hiyo ya 90 kulikuwa na Jambazi tishio mkoani Morogoro alijulikana kwa jina la Ndanje hata hivyo baadae aliuwawa na watu wenye asila kali akiwa ndani ya basi.
Umeishi mtaa gain hapa Mo Town Mafisa, Msufini, Kilakara,
Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma Road, SUA,
Vibandani, Relwe Magorofani, Kigurunyembe,
Madizini Tungi Tubuyu Kihonda.
Lukobe Kasanga, Mindu Mzumbe. Mzinga Magafu Liti Kibwe Juu ya Milima ya Uluguru Bigwa.
Misongeni Pangawe Jeshini Mzinga Jeshini Kauzeni Kingolwila Nane Nane Chamwini Mazimbi Modeko Kihonda Maghorofani? Au wapi Umeishi? Kwenye mitaa yote hiyo eneo la Kihonda Maghorofani ndio eneo ambalo Mastaa wengi wa Tanzania wamejenga hapo.
Kwa haraka haraka Mtandao huu unawataja Mastaa ambao nyumba zao zipo eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Amos Makalla.Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Marehemu Mchungaji Lwekatale, Kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime.
Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Ulimboka Mwakingwe na kocha wa Makipa wa Kagera Sugar Juma Kaseje.
Mastaa wengine wanaishi Kihonda Maghorogani ni Kiungo Punda wa Simba Mzamiru Yassin, Kiungo wa Yanga Zawad Mauya na Mwanamuziki wa muziki wa kizazi Kipya Stamina.
Kuna watu maarufu wengi wa Dar es salaam ambao
maujanja yao wamejifunzia Moro Town.
Ile kauli kwamba Moro Mji kasoro bahari nakwenda kuifuta kwa sasa tuna bahari yetu ya Bwawa la Mindu kila siku kuu familia zinakwenda kwenye Bwawa hilo kuogerea kama inavyoonekana Pichani.
Hata hivyo baadae serikali ya Mkoa ilipiga Marufu watu kwenda kuongerea kwenye Bwawa hilo ambalo Maji yake ndio ambayo wakazi wengi wa Mkoa wa Morogoro wanayatumia kunywa.
Kwa leo Makala hii ya historia ya Mkoa wa Morogoro inaishia hapa asante kwa kunisoma Maoni ushauri wasiliana nami kwa namba 0715 28 90 73
No comments:
Post a Comment