Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, January 8, 2023

UJUMBE WA NENO LA MUNGU.   MCHUNGAJI AISHAURI SERIKALI KUTUNGA SHERIA YA KUWABANA WATOTO WASIO WATUNZA WAZAZI WAO.


 

 

Na Mtumishi Dustan Shekidele,Morogoro.

 

 MPENDWA Msomaji wa Mtandao Pendwa wa Shekidele,Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo. Amani ya Mwenyezi Mungu na iwe Juu yenu, Nawasalimi katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Ama baada ya salam kama  Mitume wetu walivyodai kwamba wanaosalimiana wana Kheri kwa Mwenyezi Mungu,hivyo baada ya salamu hizo tuingie kwenye somo letu la leo Jumapili ya kwanza ya Mwaka Mpya wa 2023.

 

Somo hilo linatoka kwenye mahuri aliyotoa Mchungaji Nuhu wa KKKT Usharika wa Kihonda kwenye lbada ya kumuombea Marehemu Agnes Togolai Shekidele aliyetwaliwa na bwana Disemba 16 na kupunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele Disemba 18.

 

 lkumbukwe hayati Agnes ni mke wa Mzee Togolai Shekidele ambaye ni baba mdogo wa Mwandishi wa Mtandao huu.

 

Kwenye lbada hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu eneo la Mji Mwema Kata ya Tungi Mkoani hapa,mtumishi huyo wa mungu aliwachpa kwa maneno watoto wasiowatunza wazazi wao.

 

 

Kufuatia hali hiyo mtumishi huyo wa Mungu aliishauri Serikali kutunga sheria ya kuwabana watoto hao wanaowatelekeza wazazi wao.

 

“Biblia inasema baba na mama ni miungu yako ya duniani na ukiwaheshimu  Mungu anakuongezea siku zako za kuishi hapa duniani. Kama kunasheria imetungwa na kumkamata mzazi asiyemlea na kumsomesha mtoto wake basi itunge sheria nyingine ya kumkamata mtoto asiyewatunza wazazi wake.

 

Wazazi wengi tunawasomesha na kuwalea watoto wetu kwa upendo wetu kwao mara nyingine utakuta mzazi kule kijiji anauza shamba lake anamsomesha mtoto wake mpaka Chuo Kikuu pia kuna wazazi wengine wametelekezwa na waume zao wanawasomesha watoto kwa kuchoma mihongo au kucheza Vicoba.

 

Leo mtoto huyo kamaliza chuo kapata kazi nzuri analipwa mshahara mzuri hamjali tena mzazi wake huyo badala yake kila mwaka anaponda pesa kwenye Birthday yake kwa kuwa nunulia  Vyakula na Pombe watu wasiokuwa na jasho lolote kwenye pesa hizo huku mzazi wake  aliyemsomesha kwa shida na tabu nyingi akiteseka kule kijijini.

 

Hii sio sawa ifike mahari serikali utunge sheria nyingine ya kuwabana watoto wasiowatunza wazazi wao”alisema Mchungaji huyo na kupokea zawadi ya makofi kutoka kwa umati wa watu wa dini mbali mbali waliojitokeza kwenye Msiba huo.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...