Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, January 7, 2023

UDAKUZ SPESHO.   TIMBWILI LAIBUKA KATIKATI YA SOKO MWANAMKE AJAZA WATU AKIDAI UJIRA WAKE KWA MPENZI WAKE.


 

 

Na Mdakuzi Dustan Shekidele,Morogoro.

 

 UKISTAAJABU ya Mussa huto yaona ya Firahuni.

Msemo huo umetimia  baada ya Mwanamke mmoja anayedaiwa kufunga safari kutoka Dar Mpaka Moro kuja ‘kudanga’ kajaza  watu sokoni akimdai Pesa Mwanaume aliyelala naye.

 

Tukio hilo la kushangaza limetokea jana asubuhi kwenye duka la Mwanaume huyo lililopo eneo la Soko Kuu la Kata ya Mji Mpya.

 

 Kama kawa Mdakuzi wa Mtandao huu mwenye ‘Fan base’ kubwa  kona zote za Mji wa Morogoro alirambishwa Ubuyu huo mbichiii uliokorea rangi.

 

 Mara baada ya kutokea kwa Mtiti huo uliowaradhimu Polisi kutinga eneo la tukio baadhi ya watu walimtwangia simu Mdakuzi ambaye fasta alitinga eneo la tukio.

 

Mdakuzi huyo alipofika alishuhudia kwa mbali Difenda la Polisi likiondoka eneo la tukio na wahusika wote wawili wakielekea kituo cha Polisi.  

 

Baada ya kukosa Picha za tukio hilo Mdakuzi aliamua kuwahoji baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo walioshuhudia Live bila chenga tukio hilo.

 

 Mashuhuda wengi walikuwa tayari kuzungumzia akiwemo bibi anayekadiliwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 60.

 

 Hivyo Mdakuzi aliamua kuwapiga chini vijana na kuzungumza na bibi huyo aliyekubali kulidadavua tukio hilo kwa sharti la kutotajwa jina lake popote.

  

 MSIKIE BIMKUBWA HUYO AKITIRIRIKA.

“Vijana wa sasa  mnashida sana baada ya zogo kuw akubw ahapa dukani watu wengi tuliacha biashara zetu sokoni tukaja eneo la tukio,kwa mujibu wa huyu binti alivyokuwa akiwaeleza ni kwamba alikutana na huyu kijana mwenye hili duka kwenye Mitandao ya Kijamii yeye akiwa Dar.

 

Kwenye kuchati wamekubalia aje Moro kuumwagilia moyo amedai alivyoomba nauli huyu kijana kamwambia ajiripia akifika atamludishia.

 

Kwa upendo wa wake kwa kijana huyu bint huyu kadai amekopa nauli kwa rafiki yake kapanda basi kaja,alipofika Msamvu huyu Kijana katuma boda boda kaenda kumpokea  alipofika hapa dukani huyu Kijana kamwambia boda boda ampeleke gest ya hapo mtaa wa pili.

 

Kijana alipofunga duka kaenda kulala na bint huyo alfajiri kamuaga kwamba anakwenda kuwahi kufungua duka mida ya saa 2 atamfuata wakanywe supu.

  Ilipofika saa 4 muda wa kurejesha Chumba wahudumu walimgongea na kumuliza kama anaendelea kuwepo au la bint huyo aliwaambia anaondoka hivyo wahudumu wakadai pesa ya chumba  bint  kumua kumpigia  mwenyeji wake simu imezimwa.

 

Wenye gest wamemjia juu wakitaka pesa yao wakidai huyu Mwanaume hawamjui wanamjua yeye aliyejisajiri kwenye kitabu cha wageni  kwa maelezo ya huyu bint kalipa pesa hiyo na kuja hapa dukani kumuliza Mpenzi wake kulikoni”kasema bibi huyo na kuendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

 

“Alipofika hapa kawa mkali kaanza kuzozana na huyu kijana kwa kitendo hicho cha kumtelekeza gest kisha kumzimia simu kijana huyu naye kaja juu akimjibu kwamba hana pesa ya kuchezea kajileta  mwenyewe Moro aludi mwenyewe Dar.

 

Baada ya majibu hayo bint huyo kamua kwenda kituo cha Polisi cha Mji Mpya, chaajabu alipofika huko kaipa uzito kesi akidai kaibiwa laki nane na huyu Kijana wakiwa wamelala usiku.

 

Polisi wamefika na kumkamata Kijana huyo wakaelekea Polisi hivyo hatujui kinachoendelea huko”alimalizia kusema bi Mkubwa huyo.

 

 Toka jana mpaka leo story kubwa  sokoni hapo na tukio hilo ambapo wafanyabiashara wa soko hilo wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya tukio hilo,upande mmoja  walimlaumu  bint huyo kwa kufunga safari kutoka Dar mpaka Moro kuja kulala na mtu asiyemjua tena kwa kutumia nauli yake.

 

 Upande wa pili wengi wao wakiwa wanawake wakimlaumu  kijana huyo kwa kumfanyia ukatili  bint wawatu aliyefunga safari kwa upendo kutoka Dar mpaka Moro kutii mwaliko wa Kijana huyo aliyejenga naye urafiki kupitia mitandao ya Kijamii.

 

Si juia kwa upande wako wewe msomaji wa Mtandao Pendwa wa Shekidele uko upande gani kwenye  Msala huu au umepata somo gani juu ya tukio hili?

 

Jana majira ya saa 2 usiku Mdakuzi wa Mtandao huu alitinga kwenye duka hilo kwa lengo kuzungumza na Kijana huyo ambapo boda boda wanao egesha Pikipiki zao nje ya duka hilo la kuuza maji ya jumla  walidai  hadi muda huo kijana huyo hajarejea kwenye duka hilo.

 

 Mdakuzi wa Mtandao huu ataendelea kufuatilia udakuzi huo kwa kuzungumza na kijana huyo hivyo kama tukifanikiwa kumpata Mrejesho wa Udakuzi huu utaruka hewani Jumamosi ijayo kwenye ukurasa huu.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...