Baadhi ya waandishi wa habari wakipiga Picha ya pamoja Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa. Mh Fatuma Mwassa, Miongoni mwao ni Mwandishi wa Mtandao huu aliyesimama nyuma ya Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mzee Steven Joshua Mashishanga[mwenye skavu ya pendera ya taifa shingoni.Mwenyekiti wa Chama hicho Nickson Mkilanya akimsindikiza Mkuu huyo wa Mkoa mara baada ya kufungua Mkutano huo.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
WIKI iliyopita Mtandao huu ujitika kwenye habari ya kiuchunguzi kuelekea Manispaa ya Morogoro kuwa Jiji.
Siku moja baada ya kukamilisha kwa habari hiyo iliyoruka hewani takribani siku 3 mfurulizo, siku iliyofuata Disemba 30 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Fatuma Mwassa aliarikwa kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’.
Kabla ya kufungua Mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa alipata wasaa wa kuzungumza Machache na Waandishi hao kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro.
Miongoni mwa machache hayo Mh Fatuma alitema nyongo kuhusiana na mpangilio mbovu wa Majengo kwenye Mkoa huo uliojaliwa kila aina ya rasrimali.
” Morogoro ni Mkoa pekee ambao watu wanajenga kiholera kwenye utawala wangu hili halina nafasi yaani mtu ana amka asubuhi ana mwaga tofati popote na kuanza kujenga bila kibari cha ujenzi.
Nimebahatika kuishi mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Tabora, Geita na Visiwani hilo la ujenzi holela nimeliona hapa Morogoro, Kwa hali kama hii mkoa wa Morogoro kuendelea ni shida sana”alipigilia msumari wa Moto Mkuu huyo wa mkoa aliyewahi pia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero miaka ya 2005.
Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilim, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Fikiri Juma na Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mzee Steven Mashishanga ambaye yeye na tajiri Aziz Abood ndio walezi wa Chama hicho cha Waandishi wa habari.
Mtandao huu umekusanya matukio kadhaa kwenye Mkutano huo uliofanyika ndani ya ukumbi wa JKT Bwalo la Umwema hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao Pendwa wa Shekidele Muda wote.
No comments:
Post a Comment