Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, January 18, 2023

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA SIMBA.MZEE DALALI ANGUSHA DUA NZITO AKIMUOMBEA KULA MGOMBEA WAKE


 

 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mwenyekiti Mstaafu wa timu ya Simba Mzee Hassan Dalali mwenye koti jeusi na Bagharashia jana jioni ameongoza dua nzito kwenye tawi kuu la Simba  Mkoani Morogoro Maarufu tawi la Shujaa akimuombea kura Mgombea Uwenyekiti wa timu hiyo anayemuunga mkono Wakili Moses Kaluwa Pichani kulia Mwenye Miwani.

 

 

Baada ya Dua hiyo Mzee Dalali ambaye ni Mwenuyekiti Mstaafu wa timu hiyo alinza kumwagia sifa Wakili Kaluwa huku akiwahamasisha wanachama hao wa Simba wa tawi hilo la Shujaa kumchagua Kaluwa kuiongoza timu hiyo.

 

”Wakati nikiwa Mwenyekiti wa Simba Kaluwa na Marehemu Has Pop walinisaidia sana kwenye kazi  ya kumfunga Mtani wetu hivyo”Alisema Mzee Dalali na kupokea zawadi ya Makofi mengi kutoka wa Wanachama hao wa Simba walifulika kwenye Tawili hilo lililopo Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro.

 

 Miongoni mwa Matawi ya Simba yenye nguvu nchini ni pamoja na tawi hilo la Shujaa.

 

 Uchaguzi wa Simba umepangwa kufanyika January 29 jijini Dar es salaam na kwa sasa baadhi ya  wagombea  wanazunguka kwenye matawi ya Mikoani wakipiga kampenzi za kuomba ridhaa kwa wanachama ya kuiongoza timu hiyo kubwa nchini.

 

Habari zaidi na Picha nyingi za tukio hilo zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...