Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, December 8, 2022

SEHEMU YA 3 STORI YA MLEMAVU. MWANAFUNZI MLEMAVU WA MACHO ANAYESOMEA UANDISHI WA HABARI AFUNGUKA MAZITO.

              Hassan Muhidini akihojiwa na Mtandao huu
Mwalimu wa MSJ akimuongoza Muhidini kusoma Taarifa ya habari ukumbini
Muhidi akisoma Taarifa ya habari ndani ya ukumbi Mkubwa na wa kisasa wa MSJ
...Akisoma taarifa ya habari kwa Maalumu yanayosomwa kwa alama za Vidole
 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

MWANAFUNZI anayesomea Uandishi wa habari fani ya Utangazaji wa Luninga na Radio Mwenye ulemavu wa Macho’Kipofu’Hassan Muhidini[20]Mkazi wa Kijiji Cha Kiloka Tarafa ya Mkuyuni Wilaya ya Morogoro Vijijini amefunguka mazito juu ya uhamuzi wake huo wa  kusomea Uandishi wa habari.

 

Akizungumza na Blog Pendwa ya www.shekideletz.blogspot.com kwenye Mahojiano Maalumu Muhidini aliyejiunga na chuo hicho wiki 3 zilizopita alifunguka mazito kwenye Mahajiano hayo ambayo yalikuwa hivi.

 

Mwandishi-Habari yako.

 

Muhidini.Njema kama unavyoniona sioni naomba kukufahamu.

 

Mwandishi- Mimi naitwa Dunstan Shekidele ni Mwandishi wa habari wa Magazeti ya Raia Mwema, pia ni Mmiliki wa Blog ya Shekidele na mitandao ya Miwili ya facebook mmoja natumia jina la shekidele mkude simba na wapili natumia jina la Dustan Shekidele.

 

Muhidini- Hooo Ok na mimi ndio nasomea fani hiyo kwa sasa nikimpendeza Mungu miaka 2 au 3 ijayo nitakamilisha masomo yangu.

 

 Mwandishi- Ok karibu kwenye fani naamini kwa uwezo wa Mungu utakamlisha vyema Masomo yako, kwani unauwezo mkubwa wa akili kwa wiki 3 ulizokaa hapa Chuoni na ulivyo soma taarifa ya habari kwa weledi mkubwa ni zahiri shahiri ukimaliza Mwaka hapa Chuoni utakuwa mbali sana kimasomo.

Muhidini- Amina  

 

Mwandishi- .Naomba unipe histori ya maisha yako kwa ufupi.

 

Muhidini- Ok nilizaliwa miaka 20 iliyopita katika kijiji cha Kiloka Tarafa ya Mkuyuni  Wilaya ya Morogoro Vijijini. Kwa kuwa pale Kijijini hakuna shule inayofundisha kwa alama za Vidole wazazi wangu walinipeleka  shule ya Msingi Mazinyuko iliyopo Kilosa ambayo inadarasa la walemavu tukifundishwa kwa alama za vidole.

 

 Nipomaliza la saba nilianza kidato cha kwanza shule ya sekondani Lugoba iliyopo Chalinze Mkoa wa Pwani ambayo pia inadarasa la walemavu wa Macho tukifundishwa kwa alama za Vidole.

 

Baada ya kumaliza kidato cha 4 kwa sasa nasoma hapa Chuo cha Uandishi wa habari nimelipoti kwa mara ya kwanza wiki 3 zilizopita.

 

Mwandishi- Ok, kitugani  kilichokusukuma kusomea  Uandishi wa habari.

 

Muhidini- Swali zuri sana, sababu kubwa ya kusomea uandishi wa habari ni kuwasaidia walemavu wenzangu kupasa sauti hasa wale wenye changamoto mbali mbali ambao hawana sehemu ya kupaza sauti zao hivyo kupitia mimi nitawasaidi kupaza sauti zao kupitoa kazi  yangu ya Uandishi toka nikiwa kidato cha kwanza ndoto zangu zilikuwa hizi za kusomea Uandishi wa habari.

Mwandishi- Mimi namisoma Chuo hiki cha MSJ najua hakuna darasa la kufundisha kwa alama za Vidole je wewe unatumia njia gani kuwaeleza wakufunzi wa Chuo?.

 

 Muhidini- Ni kweli chuo hiki hakina dasara maalumu la kufundisha kwa alama za Vidole. Kwa sababau tayari najua kuandisha na kusoma kwa alama za vidole hivyo wakufunzi wananifundisha kwa kunieleza kwa maneno  nayaandika kwa alama za vidole,mfano hii taarifa ya habari niliyo soma Mwalimu kaiandaa akanisomea nikaiandika kwa mfumo wa kusoma kwa alama za Vidole.

 

 Kwenye masoma ni hivyo hivyo Notice wananisomea nandika kwa mfumo wa alama za Vidole.

 

Mwandishi- Hapo nimekuelewa Vizuri  sina swali la nyingeza hivyo mahojiano yetu yanaishia hapa asante sana kwa ushirikiano wako ahadi yangu kwako panapo majaliwa na Mwenyezi Mungu siku ukihitimu mafunzo yako nitafika kukusapoti.

 

Muhidini Hoo asante sana na Mungu akubariki sana na akufanyie wepesi kutimiza ahadi yako hiyo.

 

 Tumefika Mwisho wa mahojiano ambapo pia ndio mwisho wa stori za ndugu yetu  Muhidini, Mtandao huu unamuomba Mwenyezi Mungu amuongoze  kwenye masomo yake hayo sambamba na kumfanyia wepesi wa kupata ada kwa  kipindi chote cha miaka 3 atakapokuwa Chuoni ambapo ambapo Mwaka mmoja atapata Certificate na miaka 2 mbele atapata Diploma ya Uandishi wa habari.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...