Kwasi anaramba udogo wa Uwanja wa Saba saba baada ya kuzidiwa na nguvu wa winga wa Eleveni Killer
Kipa wa Moro Youtn Laily Laily akiwajibika gorini jana jioni
Kwasi akijianda kuingia uwanjani
Kocha Mkuu wa Moro Youth Salim Mbonde wa Mwisho kulia mwenye Kapeto akiwafuatilia Vijana wake
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Ligi ya Taifa daraja la Tatu Mkoa wa Morogoro inayocheze kwenye vituo viwili vya Manispaa na Kilombero inazidi kushika kasi.
Katika Mchezo uliopigwa juzi kwenye uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro timu ya Chamwino Ranger yeye Maskani yake Kata ya Chamwini Manispaa ya Morogoro iliichapa timu ya Kilosa United Kwa bao 2-1.
Jana kwenye uwanja huo huo wa Saba saba Vijana wa Moro Youth ‘Full Vipaji’wanaofundishwa na Kocha Salim Mbonde waliichapa timu ya Eleven Killer kwa bao 2-0.
lfahamike Mbonde aliyetokea kwenye taasisi hiyo ya Moro Youth Maarufu Moro Kids alitimkia Mtibwa B kabla ya kupandishwa kuitumika timu ya Mtibwa ya wakubwa akicheze beki ya kati, baadae kuchaguliwa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars.’
Mbonde aliyehitimu kidato cha 6 shule ya Sekondari Morogoro baada ya kufanya vizuri zaidi na timu hiyo ya Taifa Uongozi wa Simba ulivutiwa na kiwango chake hivyo kumsajiri kwenye kikosi hicho chenye Maskani yake Mtaa wa Msimbazi wenye Pilikapilika nyingi pengine kuliko Mtaa wowote eneo hilo la Kariakoo Dar.
Akizungumza na Mtandao huu Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Manispaa Jimmy Lengwe ambaye pia ni Katibu Msaidizi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ alisema ligi hiyo inacheze kwa kasi ya ajabu kufukuzana na Muda.
“Shekidele tunatakiwa kupeleka jina moja la bingwa wa ligi daraja la tatu Mkoa
wa Morogoro TFF Taifa tarehe 18 mwezi huu wa Desemba”alisema Lengwe ambaye pia
ni Mechi kamishina wa ligi Kuu Tanzania Bara.
.
No comments:
Post a Comment