.
MATHAYO 5- 13-16
“Nyinyi ni Chumvi ya dunia,lakini Chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee?.Haifai tena kabisa ila kutupwa nje na kukanyagwa na Watu.
Nyinyi ni Nuru ya Ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa Juu ya Mlima.
Wala Watu hawawashi taa na kuiweka Chini ya Pishi bali Juu ya Kiango nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Hivyo hivyo nuru yangu na iangaze mbele ya watu,wapate kuyaona matendo yenu mema yamtukuze baba yenu aliyembinguni.
Hilo ndilo neon letu la leo Jumapili ya Desemba 11-2022.
UCHAMBUZI WA NENO HILO.
Mungu kupitia kinywa na Mwanae Mpendwa wetu Yesu Kristo ambaye waumini wa dini nyingine wanamtambua kwa jina la Nabii lssa.
Aliyekubali kutoa uhai wake ili mimi na wewe tuokolewe kwenye neno hapo juu alisema kwa Mafumbo, Sasa Mtumishi wako najaribu kulifumbua fumbo hilo kwa Upeo wangu Mdogo.
Kwamba sisi Wanadam ni Nuru na Chumvi ambapo Mungu katupa upendelea wakujua mame na mabaya sambamba na kuvitawala vitu vyote vilivyopo hapa Ulimwenguni.
Sasa wewe binadamu uliyepewa Cheo hicho Kikubwa halafu unakwenda kinyume na maagizo ya Mungu hata ukirekebishwa na Viongozi wako wa dini ama wazazi wako bado hubadiliki basi wewe hufai unapaswa kutupwa nje na kukanyagwa na watu kama ile Chumvi iliyoharibika.
Kuhusu Nuru tunaagizwa na Mungu kufanya mambo mema kwa jamii na kuwa Mwanga utakaotumulikia siku tukiwa na giza, Mungu akiwa na Maana kwamba Utakapowasaidi watu wenye shida kwa maana ya kuwamulikia Nuru wakaona Mwanga kwenye maisha yao basi na wewe siku ukiwa na giza Mungu naye atakumulikia Nuru yake utauona Mwanga.
Kwenye hili Mungu katoa kalipio kwa baadhi ya matajiri kula mali zao na familia zao pekee huku wakishindwa kuwapa msaada majirani zao wanaokabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo njaa ya chakula.
Huku matajiri hao wanakula chakula na kusaza kuna tajiri mmoja Mbwa wake chakula anachokula kwa mwezi ni zaidi ya laki 4, huku Jirani yake kuna majaira anashindia uji baada ya kukosa pesa ya chakula hili ni chukizo kwa Mungu.
Kwenye neno la Mungu hapo Juu kawafumbia fumbo watu hao akisema ‘ Nuru zenu msisiweke nyumbani kwenu pekee ziwamulikie nyinyi tu bali zitoeni na nje ziwamulikiwe watu wote.”
Kwenye Biblia hiyo hiyo kuna mstari mwingine Mungu alisema, Ni heli ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia Peponi. .
Kufuatia kauli hiyo kuna mmoja wawanafunzi wa Yesu ambaye alikuwa fukara lakini kajiripua na kumuliza swali Yesu’ Mwalimu kama hivyo ndivyo Matajiri hawatauona ufalme wa Mungu?. Yesu akamjibu akiseme watakaoingia wataingia kwa Neema ya Mungu Pekee na si Vinginevyo.
Kwa leo Mtumishi wako naishi hapa Mungu akipenda tukutane jumapili ijayo kwa soma lingine.
No comments:
Post a Comment