Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, December 5, 2022

MKURUGENZI CLOUDS MEDIA AWAHASA WAHITIMU CHUO CHA UANDISHI WA HABARI MOROGORO.D

                 Wahitimu wa Diploma ya Uandishi wa habari
...Wahitimu wa Certificate ya Uandishi wa habari


Wahitimu wa Diplona wakiinamisha vichwa chini kwa dakika  1 wakimuombea mwenzao aliyefariki dunia kabla ya ndoto zake za kuhitimu mafunzi hayo ya Uandishi wa habari kutimia
lsaya Kandonga aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Clouds Media Joseph Kulangwa akizungumza kwenye Mahafari hayo
Mkurugenzi wa UTPC Keneth Simbaya akizungumza kwenye Mahafari hayo
Rais wa UTPC Deogratias Nsokolo akizungumza kwenye Mahafari hayo
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha MSJ Bujaga lzengo Kadago akizungumza kwenye Mahafari hayo
                     Vigogo wa UTPC Wakiteta jambo
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habri Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya[kushoto] akisalimiana na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania'UTPC' Deogratias Nsokolo
Dolly Mizambwa akielekea mbele kununukiwa Diploma ya Uandishi wa habari na Mkuu wa Chuo
....Wahitimu hao wakivua kofia ikiwa ni ishara ya kununukiwa Diploma ya Uandishi wa habari huku wakipigiwa Matalumbeta
Dolly Mizambwa mmoja wa wahitimu wa Diploma akirusha juu kofi yake kwenye ukumbi wa Kambarage ambapo wazawadi wake walimfanyia sherehe kabambe ya kumpongeza na Mpiga Picha Maarufu wa Mtandao huu alipewa penda ya kupiga Picha matukio yote
Wahitimu wakisakata Rhumba baada ya kuhitimu


Mgeni Rasm lsaya Kandonga akikabidhi zawadi ya Cheti cha Utumishi  bora Bujanga Kadago kulia

 Mfanyakazi wa bora wa Chuo hicho Diha Zongo akikabidhiwa zawadi ya Cheti  na Mgeni rasmi

 

 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Clouds Media  Joseph Kusaga amewashauri Waandishi wa habari wamtangulize Mungu Mbele kwa kila jambo,huku akiwataka wasijifungie kwenye fani ya  Uandishi wa habari pekee bali wajiongeze kwenye fani nyingine Sambamba na kujiendeleza kielimu.  

 

 

Big Bos huyo wa Clouds Media alitoa rahi hiyo juzi kwenye Mahafari 26 ya Chuo Cha Uandishi wa Habari Morogoro’MSJ’kwa wahitimu wa Diploma na Certificate.

 

Mahafari hayo yaliyofana vilivyo yalifanyika   kwenye ukumbi wa Chuo hicho kilichopo Mkundi Mizani ya Zamani Mkoani hapa.

 

Kusaga aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafari hayo aliwakilishwa na lsaya Kandonga ambaye ni Mkugugenzi wa TV3 na Star Bongo Clouds Media.

 

 “ Bosi Kusaga pia alinituma niwaambie kwamba Waajiri wengi siku hizi hawaangalii zaidi  vyeti pekee wanaangalia zaidi Uwajibikaji,hali ya kujitoa kwa mtu na  kujiongeza kwenye Majukumu yake ya kazi.

 

 Clouds Media tutaajiri wahitimu wawili wa kike ambao nitawataja majina hayo hapa hapa ukumbini”alisema Kandonga wahitimu hao wawili waliotajwa wametoka kwenye kundi la wahitimu wa Diploma.

 

 Mahafari hayo pia yaliyohudhuriwa  na Mkurugenzi Mkuu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania’UTPC,Keneth Simbaya, Rais wa UTPC  Deogratias Nsokolo, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Morogoro Nickson Mkilanya na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Bujaga lzengo Kadago.

 

 lkumbukwe Kadago ni Mtangazaji Mkongwe aliyewahi kutamba na Radio ya Taifa zamani RTD badae akatimkia ITV na Radio One kabla ya kuhamia Abood Media ya Morogoro.

 

Bujanga Mzee wa Mipango hakudumu sana Abood Media ambapo alirejea  Serikalini akijiunga na SUA Media akiitumikia kama Meneja kabla ya kustaafu hivi karibuni,kwa sasa Bujanga ni Mjasilia Mali akijikita kwenye Ufugaji wa Kuku wa Kisasa Nyumbani wake Kasanga.

 

Mkogwe huyo wa Utangazaji nchini Pia aliwahi kuwa Mwalimu wa Chuo hicho cha MSJ na Miongoni Mwa wanafunzi aliowafundisha kwenye Chuo hicho ni pamoja na Mwandishi wa Habari hizi Mwaka 2003 wakati huo Chuo hicho kikifanya shughuri zake Jengo la CCM Mkoa kabla ya sasa kuhamia kwenye majengo yake ya Kisasa yaliyopo eneo la Mkundi.

Kama kawada Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye Mahafari hayo ikiwemo tukio la Mwanafunzi mwenye ulemavu wa Macho;Kipofu' ambaye anawiki tatu toka ajiunge na chuo hicho alisoma Taarifa ya habari kwa Weledi Mkubwa utaona Clip Video cha tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...