MATHAYO 5-38.
“Nimesikia kwamba imenenwa Jicho kwa Jicho na Jino kwa Jino.
Lakini mimi nawaambia msishindane na mtu movu,lakini mtu akikupiga shavu la kuume mgeuzie na la pili.
Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako,mwachie na joho pia.
Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja nenda naye mbili.
Akuombaye mpe naye atakaye kukopa kwako usimpe kisogo”.Hilo ndilo neno letu la Mungu leo Desembe 4.
UCHAMBUZI WA NENO HILO LA MUNGU.
Kwenye neno hilo, Yesu hakuwa na maana kwamba mtu akikupiga kofi mgeuzi shavu la Pili hapana.
Yesu Kristo ambaye mara nyingi hutoa maneno kwa mavumbo aliwambia wanafunzi wake maneno hayo akiwa na Maana kwamba.
Watu wanapotufanyia mabaya tusilipitize mabaya bali tuwandendee mema.
Natambua hapa duniani kuna watu wetu tumefanyiwa ukati kwenye maeneo mbali mbali mfano kwenye Mapenzi, kwenye ajira zetu kwa maana tumedhurumiwa haki zetu, kwenye biashara zetu pia tumedhurumiwa na watu mbali mbali.
Tunafanyiwa ukatili huo huku tukiw ana watu wengie wanaotutegemea kama ilivyo kwenye picha hiyo mtu amemchinja ndege huyo anayetegemewe kwa chakila na Makinda yake inauma sana.
Binafsi toka natoka chuoni miaka 17 iliyopita nimefanya kazi kwenye kampuni moja kwa miaka zaidi hiyo 17 kwa weledi mkubwa kwa kumwaga Jasho na damu kama mnavyofahamu ugumu wa kuandika habari za Udaku zenye changamoito kali huku nikijiridhiki kusafiri kwa Pikipiki Wilaya karibu zote za Mkoa wa Morogoro nikitumwa kufuatia habari na mabosi wangu.
Mwisho wa siku mabosi hao hao wanakudhurumu haki zako za Msingi nimemshitakia Mungu naendelea kutenda mema kwenye kampuni hiyo na sina baya na mtu ila dhuruma hiyo imeyumbisha kundi kubwa la watu wanaonitegemea.
Niwatie Moyo wahanga wenzangu malipo ni hapa hapa duniani tuendelee kuwafanyie mema hao waliotumiza kwenye maeneo hayo niliyoyaanisha hapo juu na maeneo mengi ambayo sikuyataja.
Kwa leo Mtumishi wako naishi hapa, Mungu akipenda tukutane Jumapili ijayo kwa somo linge la neno la Mungu nawapenda wote.
No comments:
Post a Comment