Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, December 5, 2022

DENT MWENYE UPOFU WA MACHO AMESOMA TAARIFA YA HABARI KWA WELEDI MKUBWA.






 

 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro. MWANAFUNZI’Denit’ wa Chuo Cha Uanidshi wa Habari Morogoro’MSJ’ Mwenye ulemevu wa macho yote mawili ‘Upofu’ amesoma taarifa ya habari kwa weledi mkubwa akitumia alama za Vidole.

 

Dent huyo Hassan Muhidini[20] Mkazi wa Kijiji Cha Kiloka Tarafa ya Mkuyuni Wilaya ya Morogoro Vijijini,alisoma taarifa ya habari ya Luninga na Radio kwenye Mahafari ya 26 ya Chuo hicho yaliyofanyika Mwisho mwa wiki  kwenye ukumbi wa Chuo hicho kilichopo Mkundi Mkoani hapa.

 

Akizungumza na Mtandao huu kwenye Mahojiano Maalumu Muhidini aliyejiunga na chuo hicho wiki 3 zilizopita alisema

 

”Kutokana na changamoto za kiuchumia nimechelewa kujiunga na chuo  wenzangu walianza masomo muda mrefu huku mimi nikijiunga na chuo wiki 3 zilizopita na shukuru nimepokelewa vizuri, kwa muda mchache wa wiki 3 walimu wamenifundisha vizuri kama ulivyoona nimesoma taarifa ya habari ya Tv na Radio hapa hukumbini”alisema Dent huyo anayetembea kwa muongozo wa fimbo maalumu.

 

Hii ni sehemu ya kwanza ya mahojiano hayo  sehemu ya Pili itakuwa Clip Video cha dent huyo akisoma taarifa hiyo ya habari.

 

 Huku Sehemu ya 3 na ya mwisho itakuwa historia kamili ya dent huyo akielezea lengo lake Mama la kusomea Uandishi wa habari sambamba na kuzitaja shule alizosoma za alama za vidole za Msingi na sekondari akitaja pia sababu zilizopelekea yeye kupata upofu.

 

Kwa taarifa zote hizo  endelea kuwa jirani na Mtandao Pendwa wa Shekidele.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...