Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, December 14, 2022

MAMBO 3 YA MSHIRIKI WA MBIO ZA MAGARI KUTOKA MORO.

Dereva kutoka Morogoro Kelvin Taylor na Msoma ramani wake Maica Lyimo wakitimu vumbi eneo la Nane Nane Tubuyu Kata ya Tungi eneo la Mnada wa Ng'ombe

Madereva hao wakitokea Kihonda Yespa wakiwasili barabra kuu ya Moro Dar eneo la  KKKT Junior Seminary



Dereva kutoka Morogoro Kelvin Taylor akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu baada ya kuwasili hotel ya Cate

Dereva Kelvin akipongezwa na watu mbali mbali baada ya kuwasili hotel ya Cate

Kelvin kushoto akipongezwa na kaka yake baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya magari

......Dereva kutoka Morogoro Kelvin akiwa na ndugu na marafiki wakisuburi kukabidhiwa zawadi ya ushindi wa 4
Gari namba 11 la Kelvin nikiwa limeandikwa 'Mlete Mzungu'
....Kelvin akisindikizwa na makofi kuelekea meza kuu kukabidhiwa zawadi yake ya Mshindi wa 4
Mmoja wa viongzoi wa Cate Hotel akiwakabidhi zawadi Kelvin na Maica Lyimo
Kelvin akiwa na Msomaramani wake Maica Lyimo baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Mshindi wa 4

 ...Kelvin akipeleka tuzo yake kwa Masela wake wapiga kigoma cha Ulugway walifika hotel ya Cate kumsapoti Mwana Morogoro mwenzao


 

             Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Kuna Msema wa Kiswahiri unaosema mcheza kwao hutunza, Msema huo umetimia Jumamosi iliyopita kwenye mashindano ya Mbio za Mgari yaliyoshirikisha madereva 11 kutoka mikoa mbali mbali ya nchini za Uganda na Tanzania.

 

Kwa upande wa wenyeji wa mashindano hayo Mkoa wa Morogoro umewakilishwa na dereva mmoja Kelvin Taylor na Msoma ramani wake Mwana Mama wa Kichaga Maica Lyimo gari lao likipewa namba 11 ubavuni.

 

Wawakilishi hao pekee kutoka Mji Kasoro bahari walifanikiwa kushika nafasi ya 4 baada ya kuzidiwa sekunde chache na dereva aliyeshika nafasi ya 3.

 

Mwandishi wa Mtandao huu naye akiwana Pikipiki yake ya Mwendo Kasi alifanya kazi ya ziada ya kumfuatilia dereva huyo kutoka Morogoro kila eneo alilopita ambapo kwenye ufuatiliaji huo alinasa mambo makuu 3 kwa dereva huo na msaidizi wake.

 

 Mosi- Dereva huyo ndio dereva pekee aliyekuwa na msomaramani wa kike Bi.Maica Lyimo.

 

Pili -Gari la Kelvin nyuma liliandikwa maneno  ya utani ya ‘Lete Mzungu’neno hili siku za nyuma lilitamba sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii likimuhusisha aliyekuwa mchezaji wa  Simba Mzungu Dijan.

 

Tatu- Kelvin na msomarani wake waliwasili kwenye hotel ya Cate wakisindikizwa na Kigoma cha Ulugway kilichowaduwaza madereva wengine kutoka mikoa ya Dar Arusha na Kampala Uganda.

 

Baada ya Kelvin kukabidhiwa zawadi ya mshindi wa 4 alitinga kwenye kigoma hicho na kukata uno huku akiwa na zawadi yake.

 

Baadae Mtandao Mpendwa wa Shekidele utahitimisha habari hizo za mbio za magari kwa kurusha Picha za wafuasi wa dereva mmoja  kufanya kufulu ya pesa kwenye zoezi la ugawaji zawadi kwa washindi.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...