Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, December 16, 2022

JEURI YA PESA, GARI LA MASHINDANO LAMWAGIWA BIA ZA BEI MBAYA.

Kufuru ya pesa wapambe wakilimwagia bia gari la mshiriki wao





Dereva wa fgari hilo aliyefahamika kw ajina la Mswaki akishuka kwenye gari hilo baada ya kuwasili hotel ya Cate
                          Dereva Mswaki wakibebwa juju
...Mswaki na msomaramani wake wakikabidhiwa zawadi ya mshindi wa 6
                                            Cate Hotel


 

                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

JEURI YA PESA, GARI LA MASHINDANO LAMWAGIWA BIA ZA BEI MBAYA.

 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

WEWE Sema huna pesa kwa upande wako, au sema maisha magumu kwako  usiwachanganye watu wengine ambao wanapesa mpaka zile zakuchezea hovyo hovyo.

 

Hali hiyo imezihilika wiki iliyopita kwenye hotel ya  Cate iliyopo Kingolwira kando kando ya barabara kuu ya Moro-Dar walipofanyika kilele cha mbio za Magari zilizohusisha magari 11 kutoka Mikoa ya Dar es salaam, Arusha na wenyeji Morogoro huku mshiriki mmoja akitoka nchini Uganda.

 

Baada ya mshindano hayo kutamatika kwa dereva Tufail Tufail kutoka Dar kushika nafasi ya kwanza makabidhiano ya zawadi yalifanyika katika hotel hiyo ya Cate.

 

Katika hali ya kushangaza  baadhi ya watu wenye pesa  walilimwagia bia ya bei mbaya aina ya Heineken gari la dereva wao waliokuwa wakimsapoti.

 

Chaajabu licha ya dereva huyo aliyefahamika kwa jina la Mswaki kumaliza mbio hizo akishika nafasi ya moja kutoka mwisho kwa maana ya nafasi ya 6 kati ya gari saba zilizomaliza mbio hilo.

 

Kikundi hicho cha mchanganyika wa wanawake na wanaume mara baada ya dereva huyo kuwasili kwenye hotel hiyo walivamia gari hilo ambalo lilijaa vumbi na kurisafisha kwa kulimwagia bia hiyo yenye dhamani kumbwa duniani.

 

Kabla ya kufanya kufulu hiyo kikundi hicho kilimnyofoa dereva Mswaki kwenye gari na kumbeba juu juu, dereva huyo kuna  hivyo kachomoa simu na wallet mfukoni na kuvishikilia mkononi akiofia kuvipoteza vitu hivyo vya dhamani.

 

Kama hiyo haitoshi wenyepesa hao waliendelea kuonyesha jeuri ya pesa ambapo waliteka kigoma cha Ulugway kilichofika kwenye hotel hiyo kwa lengo la kumsapoti dereva wa Morogoro Kelvin Taylor aliyeshika nafasi ya 4 kwenye ,mbio hizo zilizofanyika eneo la Nana Nane Tubuyu Kata ya Tungi kuelekea Yespa Kata ya Kihonda.

 

Mapedeshee hao wa kike na kiume kutoa Dar waliwashawishi kwa  pesa wapiga kigoma hicho cha Ulugway ambao walifika kwenye hotel hiyo kwa lengo la kumsapote dereva wao pekee kutoka mkoaani kwao Morogoro.

Kufuatia wingi wa pesa walizotunza na mapendeshee hao Wapiga ngoma hao wakilikacha gari la Mwanamorogoro mwenzao na kuhamia kwenye gari la wageni hao.

 

 

Kiongozi wa kigoma hicho cha Ulugway alisikika akisema” Toka tumeanza kazi ya kupiga kigoma hichi hatujawahi kutunza pesa pesa nyingi kama leo mabibi na mabwana pesa tulizotunza na hawa jamaa tumehesani ni laki tano kasoro elfu 10”alisema kiongozi huyo huku akiwa na chupa kubwa la kinywaji kikali cha K Vant.

 

Miongoni mwa watu waliomwaga pesa nyingi kwenye kigoma hicho ni pamoja na huyu mdada aliyetinga kipensi cha Jens.

 

Ukitaka kuona Clip Video za mashindano hayo ya magari ingia kurasda za facebook kwa shekidele mkude simba na ile ya Dustana shekidele

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...