Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, December 17, 2022

KONA YA UDAKU SPESHO

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa eneo la Bwawani akitokea Chalinze Mkoa wa Pwani kufuatilia tukio la Mtu anayedaiwa kufariki dunia kishani kuoenekana Mtaani wenyewe walimwita Mzukule
Mwandishi wa habari za kiuchunguzi akiwa nje ya hospital ya Wilaya ya tukio akitoka wodini kuwahoji watu majeruhi waliojeruhiw akwenye mapigano ya wakulima na wafugaji

....Chombo ya Mwandishi wa Mtandao huu ikiwa juu la Mlima wa Ng'alo akitokea Matombo Wilaya ya Morogoro Vijijini kufuatilia tukio la baba kudaiwa kumuua mwanae akimtuhumu kuiba kiporo cha Wali wenyewe wanaiti Ubwabwa

Paparazi huyo akiwa juu ya Milima ya Uluguru akielekea Tarafa ya Mgeta Wilaya ya Movomeroakielekea Mgeta kwenye tukio la muda kudaiwa kumchinja shigo mdogo wake na kichwa kikipeleka kwa mnganga wa Kienyeji kwa imani za kishirikina ili apate utajiri
Mwandishi wa Mtandao huu akiwa eneo la hifadhi ya Mbuga ya Wanyama  Mikumi akitokea  Wilaya ya Kilombero
.....Nilirudi tena Kilosa kwenye tukio ambalo Mama anadaiwa kumchi Mwanaye Mlemavu chini wa uvungu ya Kitanda kwa zaidi ya miaka 5

Mmoja wa viongozi wa dini akiimwagia Maji wa baraka Pikipiki ya Mwanahabari huyo

.

                    Na Mdakuzi Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kama kawaida wiki nzima Mdakuzi wa Mtandao Pendwa wa shekidele husaka habari moja nzito ya Udaku na kuirusha kwenye kipengele cha udakuzi Spesho kinachoruka kila siku za Jumamosi.

Jumamosi ya leo Udaku hautaruka hewani kwani kuna udaku mmoja mkali na wakusisimua haujakamilika panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu udaku huo utakamilika jumatatu hivyo utaruka hewani jumamosi ijayo.

Ombi la Mtandao huu tuwe na subra tuendelee kula Mtori nyama tutazikuta chini

Baada ya kutokamilika kwa udakuz huo Mtandao huu hautakuacha hivi hivi utakupa nuku ya wiki inayosema.

 

Kupata na kukosa ni Majaliwa ya Mwenyezi Mungu lakini mara nyingi bahati huangukia kwa mtu anayejituma.

Hivyo hivyo Mara nyingi ajari humapata yule dereva Mzembe.

Pichani Mwandishi wa habari hizi akisafiri Wilaya mbali mbali za Mkoa wa Morogoro kwa usafiri wa Pikipiki baada ya kutumwa kazi za kufuatilia habari za kiuchunguzi na mabosi wake wa kampuni ya Global Publishers.

Kutokana na ugumu wa kazi hizo za habari za kiuchunguzi mara nyingine Mwandishi huyo hurazimika kusafiri nyakati za usiku Mnene huku akikatiza kwenye Misitu Minene kama mmoja ya Picha inavyoonyesha Pikipiki ya Mwandishi huyo ikiwa kwenye msitu mnene eneo la Mlima Ng’alo akitokea Matombo Wilaya ya Morogoro Vijijini akirejea Morogoro Mjini hiyo ilikuwa majira ya saa 3 usiku.

Picha nyingine Mwanahabari huyo akikatiza kwenye Mbuga ya wanyama wakali ya Mikumi akitokea Wilaya ya Kilombero kufuatilia habari ya kiuchunguzi. Picha no 3 Mwandishi huyo akiwa nje ya hospital ya Wilaya ya Kilosa akitoka kuwahoji majeruhi waliolazwa baada ya kujeruhiwa kwenye mapigano ya wakulima na wafugaji.

Picha no 4 Mwandishi huyo akiwa juu ya Milima ya Uluguru akielekea Tarafa ya Mgeta Wilaya ya Mvomero kufuatia habari ya kaka kudaiwa kumchinja mdogo wake na kichwa kukipeleka kwa mganga wa kienyeji kwa lengo la kujipatia utajiri wa kishirikina.

Kufuatia ugumu wa kazi hizo mmoja wa Viongozi wa dini aliguswa na kuamua kuimwagia maji ya baraka Pikipiki ya Paparazi huyo.

 

 
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...