Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, December 2, 2022

SOMO LA LEO NI :MFUMO WA AFYA NJEMA NA AFYA MBOVU



 

.

Na Daktari wa Mchongo Dunstan Shekidele.

Kawaida kila siku mtu anatakiwa kula kama ifuatavyo.

A.MFUMO WA AFYA NJEMA.

 

1.🍇kula wanga kamili Isiyokobolewa) 40% ili kuutia nguvu mwili na kufanya viungo vyote vya mwilini kuwa imara.

 

 Ukila Chips na yai la kuku aliyelitaga kwa kutumia madawa hapo huwezi kupata nguvu zozote  Mwili  zaidi ya kuendelea kujaza sumu Mwili wako.

 

2.🍇mboga na Matunda asilimia 30%,visivyoathiriwa na kemikali yoyote.Hii ni kwa ajili ya kuongeza kinga na kuimarisha kinga mwilini. [1].Mbogamboga ziliwe Rangi 2 hadi 9 tofauti katika kila mlo.

 

Kipimo ni visahani vya chai 13 kila siku. [I1].matunda yawe yaliyoivia mtini kikamilifu na yaliwe ndani ya masaa 6 baada ya kuchumwa,Zaidi ya hayo masaa virutubisho hupotea, Rangi ziwe kuanzia 2 tofauti hadi 24. Kwa nini? Kwa sababu kila rangi ina Kazi maalumu mwilini.

 

3.🍇Protini iliwe ile tu iliyosalama 20%.Hii ni kwa ajili ya kujenga mwili wa mtu na kukarabati seli chakavu(zilizozeeka), zilizoumia au kuharibika kwa sumu mbalimbali. (a).protini salama na 1 ni za mimea yaani maharage,kunde,njegele nk hii iliwe katika kila mlo.

(b).protini na 2 ni Nyama nyeupe yaani samaki asiye na sumu,kuku wa kienyeji asiyelishwa kemikali na sungura anayekula vitu vya asili. (c).

 

Protini na 3 ni Nyama nyekundu kama ng'ombe, mbuzi,kondoo nk,hii iliwe kwa kiasi kidogo Sana,angalau kilo 1 iliwe na watu kati ya 28 au 40 yaani 1:40 wakipungua Sana iwe 1:28.kwa nini?

 

Hii ni kwa sababu zao la mwisho mwilini baada ya protini kuchakatwa ni uriki asidi(tindikali) ambayo ikizidi mwilini huwa inakula uteute kwenye maungio ya mifupa na kusababisha mifupa kusagana.Pia inakula MADINI ya calcium yaliomo kwenye mifupa nakusababisha maumivu ya mifupa.Mafuta yake.

 

 Pia yanatabia ya kuganda mwilini na kusababisha lehemu(cholestrol na mwisho magonjwa ya moyo,pressure , stroke,kansa, mzio,sukari,kuharibu mfumo wa upumuaji ,figo nk.

 

4.🍇mafuta na sukari 10% tu inahitajika mwilini kwa siku, nzima yaani Mafuta 5% na sukari 5% tu.hivi ni kwa ajili ya kuutia joto mwili  na kusaidia shughuli za uchakataji chakula mwilini (metabolic activities).

 

Tukila  mlo kamili tunawajibika pia,kufanya yafuatayo 1.Ni lazima kufanya mazoezi au Kazi zinazoshughulisha mwili wote ili kutoa sumu na uchafu mwilini baada ya Kazi za kimetaboliki,hii hisaidia njia ya Mafuta na sukari yaliyozidi au yasiohitajiki mwilini uchomwa na kutolewa nje kwa njia ya jasho. Kwa lugha rahisi ni lazima kila siku utikise Mwili wako kwa kufanya mazoezi hata ya kutembea kwa miguu kwa umbali mrefu kidogo au kuendesha baiskeli kama Daktari wa Mchongo anavyofanya  kwenye Picha yake hapo juu ambapo akiwa kwenye shughulia zake mara nyingi hutumia usafiri huo wa baiskeli akipta faita kuu 2 Mosi anafanya mazoezi Pili anameck Mafuta kwenye Pikipiki yake.

 

Mara nyingi Daktari huyo wa Mchongo anatumia Usafiri wa Pikipiki akienda safari ndefu lakini kwa safari za hapa pata Mjini mara nyingi anatumia usafiri huo wa lnjini kiuno a.k.a Hanita.

 

Mbali na kufanya mazoezi ya baskeli Daktari huyo wa mchongo pia marangi hufanya mazoezi ya kubeba vyuma vizito kwenye Gym ya Bad Boy iliyopo ofisi ya CCM Kata ya Mji Mpya.

 

 Kama hiyo haitoshi daktari huyo wa Mchongo mara nyingine hufanya mazoezi ya kucheza mpira kwenye timu ya Morogoro Veterani kama anavyoonekana Pichani akijifua na timu hiyo ya Moro Veterani Uwanja wa Shujaa Ulipo Mji Mpya.

 Hajamaliza bado Daktari huyo wa Mchongo vile vile hufanya mazoezi ya Saydo Karate Do Federation Pawer Sports Club kwenye ukumbi wa Urafiki CCM Kata ya Kiwanja Cha Ndege ambapo eneo hilo pia bondi Maarufu nchini Twaha Kiduku hufanya mazoezi.

 

Hivyo kwa kufanya mazoezi hayo kwa nyakati tofauti Daktari huyo wa Mchongo juzi alivyopita uzito amejikuta amebaki na kilo 61 pekee na kwa Neema za mwenyezi Mungu toka azaliwe Daktari huyo wa Mchongo hajawahi kuugua ugongwa wa Presha wala Kisukari.

 

2.Nilazima kupata Muda wa kupumzika angalau masaa 6 hadi 8 usingizi wa fofofo bila kuwaza chochote,ili mwili upate utulivu wa kuchakata virutubisho vyote mwilini kwa ufanisi mkubwa.

 

 Matokeo ya mfumo huu sahihi wa Maisha na ulaji sahihi unaufanya mwili upate virutubisho stahiki na hivyo kudumisha afya bora.

Kwa leo Daktari wa Mchongo anaishia hapa Panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu tukutane Jumamosi ijayo kwa mada nyingine ya Afya zetu

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...