Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, November 6, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU. MTUME SULEIMAN KAMWAMBIA MUNGU AMPE HEKILA BADALA YA UTAJIRI.

Hii ni Mwaka 2016 nikipokea shukrani kutoka kwa kina Mama hawa Majane baada ya kuwapa msaada. 

 

 

                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

MAANDIKO Matakatifu yanasema Mtume Suleiman alifanya mambo mazuri yaliyomfurahisha Mwenyezi Mungu.

 

Mungu akamwambia Mtume Suleman kwa haya mema uliyonifanyia unataka nikupe nini kwenye maisha yako.?

 

Mtume Suleman alitafakari kwa sekunde kadhaa akitafakari cha kuchagua na baadae akamwambia Mungu naomba unipe hekima ya kuongoza watu watu.

 

 Mungu akafanya hivyo akampa hekima Mtume Suleiman akaongoza watu wake wengi kwa hekima.

            SWALI KWAKO NA KWANGU.

Kwa mfano leo Maisha haya Magumu tunayoishi nayo ukibahatika ukakutana na Mungu akakueleza kwamba Mwanangu kwa mema uliyonifanyika hapa duniani chagua chochote unachotaka nikupatie.

 

Je wewe utachagua nini kati ya namba hizi 5?

[1] Utajiri,

[2]Madaraka [Cheo] kazini

[3]Mume au Mke Mzuri

[4]Watoto Wazuri.

[5]Au utachagua  busara na hekima ya kuishi vyema na Jamii inayokuzunguka.?

 

Kwangu mimi nachangua namba 5 kwa maana nikiomba Mungu anipe busana na hekima kuishi vyema na Jamii inayonizunguka bila kujali hali aliyokuwa nayo mtu.

                   

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...