Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 7, 2022

MAMIA YA WADAU WA SOKA WAKIWEMO WAAMUZI WA FIFA WAJITOKEZA KUMZIKA MWANASOKA MAARUFU MORO.


Ustadh Shabani Juma aliyeinua mikono Juu akiongoza swala ya kumuombea marehemu Abdallah Edward lkambi

...Mwili wa marehemu Dulla ukiplekwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea makaburini Kolla


Raphael akiwa mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mpendwa kaka yake

Baba mzazi wa marehemnu Mzee Edwar Sebastiani lkambi akihojiwa na Mwandishi wa Mtandao huu juzi eneo la Msibani.

Mwamuzi Raphael lkambi akihojiwa na Mwandishi wa Mtandao juzi huku akiwa mbele ya jenela lillobena mwili wa mpendwa kaka yake


Baadhi ya waamuzi wakiwa eneo la Msiba kutoka kulia ni Mwarabu Mumba, Afande Josee Mshikakibendera wa FIFA ambaye pia ni Mwanajeshi wa kambi ya

Pangawe Moro, Seleman Kinugani  wa Mwisho ni mwamuzi Mstaafu Mzee Magari ambaye kwa sasa ni Mlezi wa kituo cha Soka la Moro Kids.

Baadhi ya waamuzi wakiwa eneo la Msiba kutoka kulia ni Mwarabu Mumba,
Wamama wa Mawenzi wakimbele ya kamera Mtandao huu wakimlilia Dulla Mwene
                        Raphael akimlilia kaka yake mpendwa

Mwamuzi wa ligi Kuu Raphael lkambi Maarufu Rapha Webb Jr akimlilia Mpendwa kaka yake, huku akisaidia kupelekwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea makaburini,

 






Picha nyingine lkambi akiwa kwenye michezo mikubwa ya ligi kuu, akimlima kadi nyekundu beki wa Simba lnonga

Refa ikambi kuli akimlima kadi nyekundu beki wa Simba lnonga
Mwamuzi Raphael lkambi watatu kutoka kulia akiwa uwanja wa Manungu kwenye mchezo kati ya Mtibwa sugar na Singida Big Star

 Hayati Abdallah Mwenye akiwa juu ya kaburi la Mpendwa Mama yake

              Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mamia ya Wadau wa Soka Mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Waamuzi wa Soka wakiwemo Wamuzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia’FIFA.’

 

Juzi wamejitokeza kwa wingi kumzika Kipa wa zamani wa timu ya Eleven Killer Marehemu Abdallah Edward lkambi Maarufu Dulla Mwene ambaye ni kaka wa damu wa Mwamuzi Maarufu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Raphael Edward lkambi’ Maarufu ‘Rapha Webb Jr.’

 

Ustadh Shaban Juma kutoka Madrassa ya Msikiti wa hawaya Mawenzi aliongoza lbada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwao jirani na Soko la Matunda la Mawenzi na baada ya lbada hiyo Mwili wa Marehemu uliingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Makaburi ya Kolla kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele.

 

lfahamike Ustadh Shaban Pichani mbele aliyeinua Mikoni Juu pia ni Mwamuzi wa Soka wa daraja la kwanza.

 

Akizungumza na Mtandao huu baba mzazi wa Marehemu Mzee Edward Sebastiani lkambi alisema Mpendwa mtoto wake Hayati Abdallah aliugua ghafla Alhamis na usiku wa kuamkia ljumaa alifariki dunia.

 

Eneo la msibani kulikuwa na minong’ono kwamba wazazi wa marehemu wote wawili ni Wakristo na mtoto wao Abdallah yuko  dini nyingine.

 

 Kufuatia minong’ono hiyo Mwandishi wa habari hizi alimuliza swali hilo Mzee lkambi ambalo alijibu.

 

“Mimi kama mzazi nilitimiza jukumu langu la kumlea Mwanngu kwenye  misingi ya lmani yangu ya dini ya Kikristo alivyokuwa mtu mzima kamua kuhamia dini ya Kiislam na sisi kama wazazi tumebariki hilo ndio maana umeona tunamzika kwa lmani ya dini yake aliyoichagua”alisema Mzee lkambi ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya Saba saba United ya Mkoani Morogoro iliyoshiriki ligi daraja la Pili taifa kabla ya timu hiyo kushuka daraja na kupotea kwenye ulimwengu wa soka.

 

Mara baada ya kutokea msiba huo juzi Mwandishi wa habari hizi alitembelea ukurasa wa Facebook wa Mwamuzi Raphael lkambi ambaye pia ni mdau Maarufu wa Mtandao wa Shekidele kwenye ukusara huo unaojulikana kwa jina la Rapha Webb Jr.

 

Refa huyo wa ligi kuu ya NBC anayekumbukwa kwa matukio yake Makubwa ya mawili ya hivi karibu ya kuwalima kadi nyekundu watu Maarufu Kocha wa Yanga Prof Nabi na beki kisiki wa Simba Mkongoman lnonga aliandika Maneno haya kwenye ukurasa wake huo wa Fb.

 

“Mama angu mpokee mwanao😭😭😭 uhuu ukubwa ulionipaga siuwez mama naishi kuishiwa nguvu mama 😭😭

Nenda kaka.angu🙏🙏🙏

 

Mama yao mzazi Hayati Rose Raphael Mshuhudi alifariki dunia Miaka ya hivi karibu na kuzikwa  makaburi ya Kolla Manispaa ya Morogoro ambapo hayati Abdallah enzi za uhai wake aliwahi kwenda kuhani  kaburi la Mpendwa Mama yake kama anavyonekana Pichani akiwa juu ya kaburi hilo.

 

Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe,

Tangulika kamanda Dulla Mwene tutaonana baadae nakumbuka kila nilipokuja uwanja wa Saba saba ulikuwa ukinitania pale geni huku ukiazima baiskel yangu uende kwenu Mawenzi 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...