Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, November 20, 2022

KUMBUKIZI YA KIKOSI CHA POLISI MOROGORO.


 

KUMBUKIZI

Kikosi cha timu ya Polisi Morogoro ambayo kwa sasa imehamishiwa Moshi Mkoani Kilimanjaro na kubatizwa jina jipya la  Polisi Tanzania.

 

lkumbukwe  pia awari timu hiyo ilikuwa mkoani Tabora ikiwa daraja la kwanza kabla ya kuhamishiwa mkoani Morogoro wakati huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini I.G.P alikuwa Alhaji Omar ldd Mahita.

 

Baada ya kufika Mkoani hapa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Chama Cha Soka Mkoa waliipambania timu hiyo na kufanikiwa kupanda ligi kuu.

 

 Kikosi kilichoipambani timu hiyo na kufanikiwa kupanda ligi kuu mwaka 2013 ni hiki hapa.

 

 Nawakumbuka baadhi ya wachezaji hao kwa majina kutoka kulia waliochuchumaa chini ni Detha Thomas, Ramadhan Said,Fikiri Hussein ‘Maarufu Chinga’ huyu ni mdogo wa mchezaji nyota wa zamani wa yanga Mohamed Hussein’Mmachinga’anayefuatia  jina limenitoka mbele yake ni Fred Omboka na wa mwisho ni Nassoro Dabi.

 

Waliosimama wengi nimesahau majina yao nawakumbuka wawili watatu kutoka kulia ni lssa na watatu kutoka kushoto ni Sosi. Wachezaji wote hao ni Maafande wa Jeshi la Polisi.

 

 Ramadhan Said na huyo wait hapo chini wako kitengo cha Trafick. Wengine wako Vitengo vya Upelelezi lakini kwa Fred Ombomba yeye kwa sasa ni bosi akibeba nyota 2 begani yuko kikosi cha Kituliza ghasia Mkoa wa Morogoro’FFU’ Wachezaji wengine waliokipambani kikosi hicho ambao hawapo pichani ni pamoja na Clement Bazo, Ally Moshi, lbrahim Pinto,  Mokili Rambo Fred Agayi Hamis Mpemba,Shomari Juma na John Tamba ambaye kwa sasa ni kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania.

 Kwa sasa wachezaji hao baada ya kuacha mazoezi miili yao imeumuka na baadhi yao vitambi vinamwagika

 

Hawa  pia ni waajiliwa wa Jeshi hilo la Polisi, kesho panapo majiliwa ya Mwenyezi Mungu itaruka hewani kumbuki ya Picha ya kikosi cha Reli ya Morogoro Kiboko ya Vigogo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...