Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, November 2, 2022

KUMBUKIZI. TAJIRI ABOOD ANASWA AKIENDESHA BODA BODA.


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TAJIRI anayetajwa kuwa namba moja Mkoani Morogoro Aziz Abood, amesaswa akiendesha boda boda.  

Abood ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini alinaswa na Mwandishi wa Mtandao huu akiendesha boda boda muda mfupi baada ya kugawa boda boda kadhaa kwa madereva wa boda boda kwenye Jimbo lake la Morogoro.

 

 Kabla ya kukabidhi boda boda hizo kwa Viongozi wa chama cha waendesha boda boda Manispaa ya Morogoro, Abood alizindua boda boda hizo kwa kuendesha Pikipiki Moja kama anavyoonekana Pichani akipiga gia.

 

Tajiri Abood anayemiliki Viwanda, Malori, Mabasi na Vyombo vya habari alikabidhi Pikipiki hizo kwenye ofisi za Chama Cha boda boda zilizopo Mji Mpya eneo la Kidongo Chekundu.

Pichani anayemshuhudia Abood ni Katibu wa Chama Cha boda boda Wilaya ya Morogoro  Juma Mbega, tukio hili limefanyika takribani miaka 5 iliyopita.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...