Mandonga kushoto akimpigia Saluti Richi kwa kufunga rasta ndefu
Richi akimuonyesha Mwandishi wa Mtandao huu anavyobadilisha style za ufungaji wa nywele zake
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
BONDIA Maarufu kwa sasa nchini Tanzania Karim Mandonga’Mtu hatari’ambaye ni Mpiga debe wa Stend ya Mabasi ya Mikoani ya Msamvu, alianza uchakaramu wake muda mrefu kabla ya kuendeleza na sasa kuuvaa Umaarufu mkubwa nchini kiasi cha kuzoa umati mkubwa wawatu kwenye mitaa mbali mbali nchini.
Mandonga kushoto akipozi mbele ya kamera za Mtandao huu takribani miaka 7 iliyopita akiwa na mpiga debe Mwenzake Richard Maarufu ‘Richi Nywele’ wakiishangilia timu yao ya Terminal inayomilikiwa na wapiga debe ‘Salange’ wa Stend ya Mabasi ya Mikioni ya Msamvu Morogoro.
Timu hiyo ya Terminal ilishiriki michuano ya Ndondo Cup iliyofanyika Uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro, ambapo Mandonga baada ya kumuona Mwandishi wa Mtandao huu uwanjani hapo alisema.
” Shekidele nipige Picha na Mwanangu Richi nikimpigia saluti kwa kufunga rasta ndefu pingeni kuliko mtu yoyote hapa Morogoro”alisema Mandonga na Mwandishi wa Mtandao huu alitii ombi la bondia huyo.
Baada ya kupiga Picha hiyo Mwandishi wa habari hizi alimhoji Richi juu ya nywele zake hiyo ambapo alipoulizwa umri wa nyweke hizo alisema.
” Shekidele nywele hizi zinaumri ya miaka 14 kwa miaka yote hiyo sijawahi kuingia saloon yoyote”alisema Richi na kumuonyesha Mwandishi huyo style mbali mbali za ubanaji wa nywele zake.
Juzi Mandonga alinaswa na Mtandao huu katikati ya Mji wa Morogoro akizungukwa na kundi la watu wakigombea kupiga naye picha.
Baada ya kuona mashabaiki wake hao wanazidi kujazana na kupoteza muda wake aliwachenchia na kuwapiga mkwara wa utani akisema.
” kweli nyinyi ni mashabiki wangu damu damu nashukuru kwa hilo nawaomba radhi nimeshapiga picha na watu wengi naona mnazidi kuongezeka muda unakwenda shughuri zangu zimesimama hivyo anayetaka kupiga picha na Mandonga Mtu Kazi muda huu anipe buku moja.”
Kwa sasa Mandonga yuko kwenye mazoezi Makali akijiwinda na mpambano wake ya tarehe 25 mwezi huu kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
No comments:
Post a Comment