...Akiimba Tunda Spesho
...Akishirikiana kuimba na waimbaji wa Band ya Maisha Mapya
......Akiimba wimbo wa kilo cha Yatima
...Akicheza na wanenguaji wa band ya Maisha Mapya
Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.
Shoo ya pamoja ’Korabo’ya Mwamamuziki Mkongwe nchini Muumini Mwijuma iliyofanyika Mwishoni mwa wiki imeacha gumzo kwa mashabiki wa Muziki Mkoni Morogoro wakiwemo wanamichezo wa Bandari kutoka Mikoa mbali mbali nchini waliokuwa wakishiriki michezo ya Bandari mkoani hapa.
Mwijuma ‘Mzee wa Tunda Spesho’ aligonga Korabo hiyo na Vijana hao Machachari wa Band ya Maisha Mapya ya Mkoani hapa, Octobar 1 kwenye ukumbi wa Bwalo la Umwema unaomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa’JKT.’
Katika Mpambano huo Vijana wa Maisha Mapya walianza kupanda jukwaani majira ya saa 2 usiku wakagonga nyimbo 4 mfurulizo,na badae akapanda Mzee wa kazi Mwijuma anayetamba na Kibao chake cha Kilio cha yatima.
Akiwa na vazi lake la Kaunda Suti lenye ufito wa bendera ya Taifa ya Tanzania kabla ya kuimba Mwijuma alitoa tangazo kwa Mashabiki akisema.
”Mwezi uliopita nikiwa na rafiki yangu Ally Choki tumetoa nyimbo mpya ambazo kwa sasa ziko YouTube na kwenye lnstagram yangu.
Pia kwa sasa natoa huduma kwenye sherehe mfano harusi na Send Off ukiwa na shughuri yako nipigia kwa namba zangu hizi[kazitaja zaidi ya mara 3] ukipiga simu iwe kwa mambo ya kazi ninamke mmoja ninayempenda lakini dini yangu inaniruhusu kuongeza mwingine.
Hivyo Mwanamke nitakaye muelewa ni yule mwenye kisima cha mafuta ambaye nitakuwa na gemu Mafuta kwake,kinyume na hapo mimi sina Maisha kazi yetu ni hii hii ya kuimba tukiunga unga kipato changu kinanitosha na familia yangu pekee sina pesa za ziada za kugawa hovyo”alisema Kocha huyo wa duni.
Kauli hiyo iliibua Minong’ono mingi ukumbini kila mtu akisema lake hasa wanawake ambao wengi wao walikopi namba hiyo ya Muumini baada ya taarifa hiyo ya Mwisho aliyoitoa Kocha wa dunia Mlala nje aliwashuhudia baadhi wanwake wakifuta namba hizo huku wengine wakiendelea kuzisevu kwenye simu zao.
Kweli kwisha kupo Kocha wa dunia kutoka kuimba band kubwa nchini kama Vile Twanga Pepeta, Mchinga Sound, Extra Bongo. ‘So Far’ kwa sasa unaomba kazi ya kuimba kwenye Send Off na Harusi.
Kinacho mbeba Muumini si mjivuni wala mtu wa Malingo anafanya kazi popote na bei zake ni maelewano mtu yoyote anayemuhitaji kwenye Sherehe yake awasiliane na Mtandao huu.
Katika korabo hiyo kali kiingilio kilikuwa bi buree
No comments:
Post a Comment