Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, October 8, 2022

MWANDISHI WA HABARI AFUNGA PINGU ZA MAISHA KWA D.C

Msajiri wa ndoa kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya akiwapa mawaidha wana ndoa hao
                                 ...Wakila kiapo cha ndoa

                              ...Wakisaini vyeti vya ndoa


                            ...Wakivishna pete za ndoa


Msajiri wa ndoa akipiga picha na maharusi pamoja na wasimamizi wao maharusi
...Maharusi wakitoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya zoezi la kufunga ndoa kukamilika.
 


 

.            Na Dunstan Shekidele,Morogoro

 

 MWANDISHI wa habari Simon Nkongolo juzi ameukacha ukapera na kujiunga na timu bora ya wanandoa baada ya kufunga ndoa na Mpenzi wake wa siku nyingi Juliana Thomas.

 

Paparazi huyo alipasha Moto kiporo chake hicho Octobar 5 Majira ya asubuhi kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro na kufuatiwa na sherehe kabambe iliyofanyika nyumba kwao Nane nane Oil Com.

 

Simon alihitimu Chuo Cha Uandishi wa habari Morogoro ‘MSJ’Pamoja na Mwandishi wa habari hizi na wawili hao walipangiwa kwenda Fild gazeti la Majira jijini Dar.

 

Baadae Simon aliachana na kazi ya Uandishi wa habari akatimkia serikalini na kupata ajira ya Afisa Mtendaji kabla ya kuachana tena na kazi hiyo na kuingia kwenye shunguli zake bonfsi za biashara anazoendelea nazo mpaka sasa akishirikiana na mkewake huyo aliyeishinaye kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya wawili hao kukubalina kufunga ndao juzi.

 

Mtandao huu unawapongeza maharusi hao na kuwaombea kwa Mungu azidia kuwabariki na kuwaonyesha njia sahihi za kupitia kwenye maisha yao ndoa.  

             USHAURI KWAO.

Kwenye ndoa sio Peponi kwamba kila siku mtakuwa na furaha hapana kunanyakati za furaha na nyakazi za machungu hivyo mnapaswa kuvumiliana kwenye nyakati zote.

 

Tunaamini kama mmeweza kuvumiliana kwa zaidi ya Miaka hiyo 10 mlioishi mataendelea kufanya hivyo kwa siku zote za mbeleni mpaka hapo Mungu atakapowatenganisha kwa Mmoja wenu kutangulia mbele za haki.

 

Katika harusi hiyoMpiga Picha wa Mtandao huu anayetumia kamera za kisasa ndiye aliyepewa jukumu na familia hiyo kupiga Picha matukio yote. Wanandoa hao ambao pia ni wadau wakubwa wa Mtandao huu wa shekidele walikubali jambo lao hilo jema liruke hewani kwenye Mtandao huu kuudhihirishia uma kwamba wawili hao si wachumba tena bali ni mke na Mume.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...