Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, October 6, 2022

MANDONGA MTU KAZI KAREJEA TENA NYUMBANI MOROGORO.


 


                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Mbondia aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini kwa maneno yake ya shombo Karimu Mandonga Novemba 25 anazichapa na Bondia Said Mbelwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. 

 

Kila anapopiga Mandonga ambaye ni Mpiga debe Maarufu was tend ya Mabasi Msamvu huuwa anakuwa na maneno ya Mkwala kwa Mpinzania wake akiitia kauli mbio yake  ‘Slogan’ 

 

Mandonga ‘Mtu Kazi’kwenye pambano lake la Kigoma alikuja na Slogani ya’Nitampiga Mpinzani wangu kama napiga Ngoma’ juzikati kwenye Pambano lake la Mtwara alikuja na Slogani nyingine ya ‘Nitampiga Mpinzani wangu kama kaniibia Mke wangu’ Swali mpambano wake wa Novemba 25 atakuja na Slogani ipi wa kumtisha mpinzani wake?

Katika gemu hiyo Twaha Kassim Maarufu Tewaha Kiduku atakichapa na Mzungu huku Abdallah Pazi Maarufu Dulla Mbabe atakipiga na Mbia Kanku

 

Baadae Mwandishi wa Mtandao huu atakatiza kwenye maskani ya Mandonga Msamvu Stend Jumba la Mawe kuzungumza na Mandonga juu ta Pambano lake hilo na slogani atakayokuja nayo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...