Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, October 16, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU. MTUMISHI WA MUNGU ATOA USHUHUDA MZITO MSIBANI.

Mwinjilisiti Anania Nyangasa akitoa ushuhuda huo huku akionyesha Jeneza la Marehemu

 

 

         Na Dunstan Shekidele,Mikumi Morogoro.

Mwanzoni mwa  wiki hii Mtumishi wa Mungu wa Mtandao huu alihudhuria Msiba wa Mama mmoja Maarufu sana Jimbo la Mikumi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.

 

 lbada hiyo iliyohudhuriwa na watu wengi Maarufu akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Wafanyabiashara Maarufu kutoka Morogoro Mjini Pamoja na Wanajeshi ilifanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Makazi ya Wanajeshi wa JWTZ Kambi ya Mikumi kando kando ya barabara kuu ya Kuelekea Kilombero.

 

Kwenye Mahubiri yake  Mtumishi wa Mungu wa Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mikumi Mwinjilisti Anania Nyangasa[Pichani] alitoa ushuhuda Mzito wa marehemu huyo.

 

” Juzi  ljumaa Mwenyekiti wa Jumuiya ya eneo hili alinipigia simu akanijuza juu ya Kifo cha Mama yetu, naomba nitoe ushuhuda wa kweli wa Mama huyo aliyelala hapa mbele yangu kwenye jeneza hili.

 

Kama tunavyofahama mama yetu alikuwa muumini mzuri pake kanisani kwetu pia tunafahamu siku za hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbali mbali.

 

 Kwa hali hiyo Vikundi mbali mbali kutoka pale kanisani walikuja kumfariji hapa nyumbani, kwenye hicho vikundi kuna mwanakikundi mmoja aliangusha Pesa elfu 10 hapa nyumbani Sebreni.

 

Baada ya wanakikundi  kuondoka  masaa kama 5 mbele Mama huyu [anamtaja jina]kaikota pesa hiyo na siku iliyofuta kakodi Bajaj kwa pesa zake kaja kanisani kaniambia Mtumishi kuna wanakikundi  walikuja kunitembelea  mmoja wao kaangusha hii pesa hivyo naikabidhi kwako uwatangazie akipatikana mwenyewe umkabidhi haki yake.

 

Niliwaita wale wana kikundi nikawatangazia wote wakamtaja mwenzao aliyeangusha pesa hiyo nikambidhi mbele yao kwenye maelezo yake mmiliki wa pesa hiyo alisema wakujua kama iliangushwa pale nyumbani alihisi aliangusha njiani wakatika wakielekea kwa Mama huyu na kwamba alishakata tama ya kuipata.

 

Kwa  pamoja wanakikundi hao waristaajabu sana uaminifu wa Mama huyu wako hapa wanathibitisha hili ninalosema”alisema Mtumishi huyo wa Mungu na kuongeza kudadavua.

 

Baada ya kupokea taarifa za kifo cha Mpendwa wetu Moja kwa moja nilikumbuka tukio hilo la uhaminifu wake huo ambao kwenye dunia ya sasa ni wachache sana wanaoweza kurejea pesa au kitu waliookota pasipo kuonekana.

 

Hivyo kupitia uhamini wa Mama huyu kwenye mahuri  kwenye lbada ya Msiba wake nimesukumwa na roho Mtakatifu kusoma neno kutoka Ufunuo 2-10 mmoja wetu asome neno hilo.”alisema Mwinjilisti huyo ambapo Mwanakwaya mmoja alisoma neno hilo kama ifuatavyo.

 

“Usiogope Mambo yatakayokupata tazama,huyo ibilisi atawatupa baadhi yenu  gerezani ili mjaribiwe,nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi.

Uwe Mwaminifu hata kufa nami nitakupa taji ya uzima.”

 

Kwangu mimi huu ndio Mstari niliokabidhiwa na Mwalimu wangu wa Kipa lmara Mchungaji Christopher Samwel kuusoma kwa kichwa mbele ya kundi la waumini wa Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mji Mpya Morogoro Mjini. lfahamike kila dent aliyehitimu Mafunzo ya Kipa lmara moja ya kipimo anachopewa ni kuukariri Mstari wa Biblia na kuutamka kwa kichwa mbele ya waumini.

 

 lbada hiyo ya Kumuombea Marehemu wetu ilivyotamatika  Mwandishi wa habari hizi alimfuata Mwinjilisiti Nyangasa na kumshuhudia jambo hilo kwamba Mstari huo aliousoma ndio Mstari  wake wa Kipa lmara aliopewa na Mchungaji Christopher ambaye kwa miaka ya hivi karibuni alihamishiwa Usharika wa Mikumi kabla ya hivi karibuni kurejeshwa Usharika wa Mji Mpya na kupewa cheo cha Ukuu wa Jimbo la Morogoro kabla ya kustaafu Mwaka Jana.

 

Mstari huo Ufuno wa Yohana 2-10 uko kichwani kwangu toka nilipopokea Kipa lmara mwishoni mwa miaka ya 80 kwa msaada wa Mungu nitaendelea kuwa nao kichwani kama moja ya dira ya maisha uyangu mpaka hapo kifo kitakapo ni fika.

 

Swali Kwa waumini wenzangu wa dini ya Kikristo haijalisha dhehebu lako je unaukumbuka Mstari wako wa Kipa na unakuongozaje kwenye Maisha yako?

 

Mara baada ya lbada hiyo kukamilika safari ya Kuelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro kumpunzisha Mpendwa wetu kwenye nyumba yake ya Milele ilianza kwa Msafari wa zaidi ya magari 4 na kwamba siku iliyofuta tulimpunzisha Mama yetu kwenye nyumba yake ya Milele.

 

 “Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe,Tutaonana baadaye Mpendwa wetu”

 

Kwa leo mtumishi wako naishi hapa Mungu akipenda tukutane Jumapili ijayo kwa soma lingine la Muumba wetu.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...