Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, October 5, 2022

UDAKU SPESHO.WATUA KWA MZUNGU


 


Na Mdakuzi wetu.

Wiki iliyopita mchezo mmoja wa kigeni Mzungu anayecheza soko la Kulipwa kwenye moja ya timu kubwa nchini alidaiwa kutoweka kambini bila ruhusa ya Uongozi.

 

Mtasha huyo baada ya kuchomomoka kambini kimagumashi kituo cha kwanza alitua kwenye Mitandao yake ya Kijamii akitoa sababu za kujiondoa kwenye chama hilo kubwa nchini.

 

 Huko kwenye Mitandao ya Kijamii Mzungu huyo hakufafanua zaidi sababu zilizopelekea kutoweka kambini alisema mameno macha tu akidai Mwajuli wake amekiuka sehemu ya Mkataba wake.

 

Baada ya taarifa hizo kutembea kwa kasi ya ajabu kwenye Kijiwe hicho cha Mitandao ya Kijamii watu wengi waliibuka kila mtu akisema lake juu taarifa hiyo ya Mzungu.

 

Kila mtu alisema lake huku wengine wakidai Mzungu huyo aliamua kujitoa kwenye timu hiyo baada ya baadhi ya wachezaji wenzake kumnyima Pasi za mwisho za kufunga mabao’Assist.’

 

Kama ni kweli taarifa hizo Mdakuzi wa Mtandao huu anamjibu Mzungu huyo kwamba Upewe Pasi wewe ni Dobi wa kupiga Pasi nguo au?         

              UDAKUZI NAMBA 2.

Watu wengi wanasema kile wanachoamini kwamba Maisha ni Popote.

 

Mdakuzi wa Mtandao huu anapingana na watu wenye fikra hizo kwa hoja kwamba Maisha sio Popote kama maisha ni Popote basi peleka Kitanda  chooni ukaishi huko.

 

Maisha ni upambanaji ukifanikiwa ndio unaweza kutamka kauli hiyo ya Maisha Popote kwa kinywa kipana.  

 

Mwenye pesa akiamua sasa hivi anakodi ndege ana kwenda kuishi jiji la Maraha la London Uingereza.

 Kwa upande wako mwenzangu na Mimi Kama huna pesa hata nauli ya dala dala ya kwenda Kihonda huna halafu unasema Maisha Popote pambana ndugu yangu Mchani Pesa.

 

Kwa leo Mdakuzi wa Mtandao huu anaishia hapa tukutane wiki ijayo kwa udakuzi mwingine mkali zaidi ya huu.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...