Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, October 17, 2022

TIMU YA MORO KIDS LEO IMETWAA UBINGWA WA KOMBE F.A

                                     Kikosi cha Moro Kids


                           Kikosi cha Kihonda United



























 


  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Timu ya Moro Kids  imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya F.A Maarufu ‘Azam Sport Federation Cup 2022’ngazi ya Wilaya.

 

Vijana hao wa Moro Kids  kutoka kituo cha kukuza na kuibua Vipaji Mkoa wa Morogoro cha Moro Youth  imetwa ubingwa huo baada ya kuichapa timu ya ngumu ya Kihonda United kwa bao 2-0 kwenye mchezo wa fainali  uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.

 

Taarifa zilizopatika uwanjani hapo zilidai kwamba kufuatia wilaya nyingine za Mkoa wa Morogoro kushindwa kuandaa michezo hiyo ya F.A hivyo Moro Kids moja kwa moja wameteuliwa kuuwakilisha Mkoa wa Morogoro kwenye michuano hiyo inayoshika nafasi ya pili kwa ukumbwa nchini ikitanguliwa na ligi kuu ta NBC.

 

lfahamike bingwa wa michuano hiyo ya F.A anapata tiketi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya shirikisho barani Afrika. Huku bingwa wa ligi ya NBC akiiwakilisha nchi kwenye ligi ya Mabingwa barani Afrika.

 

 lkumbukwe Moro Kids inatajwa kuzalisha wachezaji wengi nyota wanaotamba kwa sasa kwenye timu mbali mbali za ligi kuu nchini.

 

 Baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Dickson Job, Kibwana Shomary na Kipa Abuutwalib Mshery wanaokipiga Yanga.

 

Shomari Kapombe na Mzamiru Yasini wanaokipiga Simba, Nickson Kibabage anayekipiga Mtibwa Sugar, Jamal Masenga anayekipiga Tanzania Prisons na Hamad Waziri’Kuku’ anayekipiga Mbeya City.

 

Wengine ni Shiza Kichuya anayekipiga Namungo ya Lindi,  Juma Abdul anayekipiga Singida Big stars na Hassan Kessy anayekipiga Dodoma Jiji.

Huku asilimia 70 ya wachezaji wa timu ya Mtibwa B waliotwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vijana wa chini ya miaka 20 ‘Under Twenty’ kwa mwaka wa 4 mfurulizo wakitoka katika kituo hicho cha Moro Youth.

           

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...