Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, October 2, 2022

MUNGU KATOA AGIZO KWA WATU WAKE.

  Kabla ya kusoma agizo hilo la Mungu hapo chini soma taarifa hii fupi inayomuhusu ndugu yetu Matama Pichani kwa mkasa mzito aliopitia.

 Kuna siku Mwandishi wa Mtandao huu  alimtembelea rafiki yake mkubwa Mohamed Athuman Matama ambaye ni mlemavu wa Miguu. 

Alipofika kwenye nyumbani aliyopanga  Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Mkoani hapa,kwa lengo la kumpa pole ya kuibiwa baiskeli yake ya mataili 3 na Vibaka  walioikata  Vipande vipande na kwenda kuuza Vyuma Chakavu. 

Shekidele alipofika kwenye nyumba hiyo siku hiyo ilinyesha Mvua alimshuhudia Matama anayeishi chumba cha uani na Mkewe Bi Maua Said akiogelea kwenye dimbwi la Maji ya Mvua akielekea Msalani umbali wa kama miguu 30 ya mtu mzima.

 lfahamike choo hicho hakiukuelezwa vizuri juu na chini hakikusakafiwa hivyo maji mengi ya Mvua yaliingia ndani ya choo hicho na kuzalisha tope zili ambapo ndugu yetu huyo anayepembea kwa mikono analazimika kulivaa tope hilo kwa mikono yote 2. 

Kitendo hicho kiliumiza moyo wa Mwandishi wa Mtandao huu ambaye alimuomba Matama kwa ridhaa yake kama atakubali kupigwa Picha kwenye eneo hilo na kuposti kwenye  Mtandao huu kwa lengo la kuendesha harambee ya kumjenga nyumba Mpendwa wetu huyo. Matama na mkewe walikubali ombi hilo ambapo Picha hii niliipositi kwenye Mitandao yangu ya Kijamii na kuendesha harambee ambapo wadau wengi wa Mtandao huu waliosambaa duniani kote baada ya kusoma taarifa za tukio hilo na kuitazama picha hii wengi waliguswa na kuchangia pesa zilizosanikisha kununua Kiwanja Maeneo ya Kichangani. 

 Huku mafundi wengi baada ya kusoma taarifa hiyo walijitolea kujenga nyumba hiyo bure akiwemo lnjinia Mzee Husema alijitolea kuchora ramani bure kama anavyonekana Pichani akisaidiwa na Mwandishi wa Mtandao huu.lnauma sana miezi michache mbele baada Mzee Hussein alifariki dunia. 

Mwandishi wa habari hii aliendelea kuspoti harambee hiyo kila wiki na wadau wangi wa Mtandao huu walichangia na kufanikisha kukamilika kwa nyumba hiyo ambapo kwa sasa ndugu yetu Matama  na familia yake washahamia kwenye Mjengo huo wa kifahari uliojengwa kwa wadau wa Mtandao wa shekidele. 

Mtandao huu Milele na Milele utaendelea kuwashukuru watu wote waliojitolea kujenga nyumba ya Mpendwa wetu baada ya kuwapitsiha kwenye taarifa hiyo fupi sasa soma ujumbe wa Mungu hapo chini.


LUKA 6-38

“Wapeni watu vitu nanyi Mtapewa Kipimo cha Kujaa na kushindiliwa na kusukwa sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa kifuani Mwenu, Kwa kuwa kipimo kile kile Mpimacho ndicho Mtakachopimiwa”Hilo ndilo neno la Leo Jumapili ya Octobar 2.

 

 Kwa leo sina cha kuchambua juu ya neno hilo la Mungu, Mwenye Masikio na asikie asiye na Masikio………]

.......Mwandishi wa Mtandao huu na Matama wakiwa na pesa mfukoni wakielekea Kichangani kununua Kiwanja.
....Pichani Matama akimkabidhi Pesa mwenyekiti wa serikali ya Mtaa ambaye baaadae akiwa kama shahidi namba moja alimkabidhi pesa hizo mmiliki wa kiwanja Mzee Mbezi aliyeshika paji la uso
......Marehemu lnjinia Mzee Hussein kulia akipima nyumba hiyo baada ya kuchora ramani kushoto Mwandishi wa Mtandao huu akimsaidia kushika kamba
.....Baada ya mchoro kukamilika Mwandishi wa Mtandao alishiriki kuchimba Msingi
....Mtu kazi Matama naye hakuwa nyuma licha ya ulemavu wake alishirikiana na mimi kushimba Msingi huu
.....Baada ya kutumiwa pesa na wadai wa Mtandao wa Shekidele tulinunua Mifuko ya saruji kwa kutumia uwafiri wetu kwa maaba ya Pikipiki ya Shekidele na baiskeli ya Matama tukiokoa pesa ya kukodi gari au Toyo
....Tumewasili nyumbani kwa Matama Mtaa wa River Side tukilakiwa na Mkewe Bi Mau Said
.....Mwandishi wa Mtandao huu akimkabidhi pesa zilizotumwa kwenye simu ya Mwandishi huyo kutoka Marekani kwa mdau wa Mtandao wa Shekidele
....Matama akishuhudia umamaji wa Mjengo wake ukiendelea chini ya lnjini Hayati Mzee Hussein Mungu amrehemu
....Mtu kazi Matama akipanga tofari za kuchoma baada ya hatua ya ujenzi wa Msingi kukamilika
....Ramani inasoma choo ndani matama anaishi kwenye chumba Master
///,Mungu ni Mwema wadai wa Mtandao wa Shekidele pande zote za dunia hasa watanzania wamekamilisha hatua ya boma
 

                             ....Hatua ya kupaua

 
Tumeshapaua badae tumeweka madirisha na Milango pamoja na Tyles kwa sasa tumeshajaza fomu Tanesko na ldara ya maji tunasubiri kuunganishiwa hudmu hizo. Wadau wa Mtandao wa Shekidele Mungu awabariki sana wote waliojenga nyumba hii.
......Mwandishi wa Mtandao huu hakuishia kwa Matama  tu alitoa Misaada kwa watu mbai mbali wenye uhitaji wakiwemo watoto yatima, hakuna mtu aliyefirisika kwa kuwasaidia watu wenye uhitaji


 Mwandishi wa Mtandao huu kulia akimkabidhi Mkurugeni wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mkitunda Bi Magreth.

Naposti hivi sio kwa jivuna bali ni kwa lengo la kukumbushana kwamba kuna wenzetu wanahitaji Misaada yetu mimi sina kipata kikubwa wala maiya yangu ni yakiwango cha chini sana Mungu mwenyewe anajua lakini kidogo hicho nasukumwa na moyo wangu kusaidia wenzangu duniani tunapita mali na pesa tutaziacha tutakwenda na roho pekee.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...