Wanenguaji wa Waluguru Og wakiwajibika juzi jumapili
Rapa wa band hiyo Jonhcena Sukari akiwajaza mzuka wanenguaji
Mpiga Tumba nyota wa band hiyo Baloteli alipoona kamera za Mlala Nje kaweka pozi kama yuko Location
Prezedaa wa band ya Waluguru Killer Boy mwenye nguo nyeusi akiongoza safu ya waimbaji wa band hiyo juzi jumapili
Hawa sio TMK Wazee wa Mapanga shaa huyu ni mnenguaji fundi wa band ya Waluguru Original akifanya yake ile ile
Mnenguaji Kipenzi cha wana Morogoro Sinyorita akiwajibika jukwaani wiki end iliyopita
Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.
Band kubwa mkoani Morogoro Waluguru Original inayomilikiwa na Jeshi la Mtu mmoja Deogratius Aruphonce Maarufu ‘Killer Boy’na Band ya Maisha Mapya inayomilikiwa na jeshi la watu wawili Joshua Malekele’na Abubakar Pugi wameingia katika vita ya kuchukuliana wanamuziki kama timu za Simba na Yanga.
lkumbukwe miaka ya hivi karibuni Mchezaji Bernard Morrison alitoka Yanga na Kujiunga na Simba kabla ya Msimu huu kutoka Simba na kureja nyumbani Yanga.
Wiki mbili zilizopita Mlala nje alishuhudia band ya Maisha Mapya ikimtambulisha Mwimbaji wa kike kutoka band ya Waluguru Og, juzi jumapili Mlala nje alitinga kwenye shoo ya Waluguru Og na kushuhudia Mpiga bess Maarufu wa band ya Maisha Mapya Samwel Maarufu ‘Sam Bass’akiwajibika kwenye jukwaa la band hiyo.
Mlala nje alimvaa mpiga bass huyo ambapo alipohojiwa alisema” Shekidele kwa sasa nimejiunga na Waluguru nimewakimbia Maisha Mapya nimekuja huku kutafuta changamoto Mpya za kimaisha”. Alisema Samu.
Usiku huo huo Mlala nje alimvutia waya Joshua Maarufu Joshkera ambapo alipoulizwa alithibitisha Sam kutimka kwenye band yake.
“ Ni kweli Shekidele Samwel sio Mwanamuziki wetu tena nafasi yake tumempata mkali wa bass nchini Papaa Sembuche” alisema kiongozi huyo Maisha Mapya Wana ‘Full Vipaji.
Katika shoo hiyo ya Waluguru kama kawaida
wanenguaji nyota wa band hiyo wakiongozwa na Mrembo Sinyorita waliuwasha moto
mkali na kukong’a nyoyo za mashabiki kibao waliofulika kwenye ukumbi huo wa Florida
uliopo jirani na Stend ya Mabasi ya Mikoani ya Msamvu.
No comments:
Post a Comment