...Baada ya Suma kunyanyua mpira juu akiusubiri huku mabeki hao wakiendelea kumchunga
...Mpira umeshatua na kaendelea kumiliki yeye akianza safari zake kama lnonga wa Simba Kamshindwa nyinyi mabeki wawili mtamuweza Suma?
....akipa wa Sarange akinyaka mpira huku akimtazama Suma
...kiungo fundi wa Sarange Jerry Santo ambaye pia aliwahi kuzitumikia timu kubwa za ligi kuu akitoka uwanja jana
......Kwa uapnde wa Wakushi pia alikuwepo Staa wa Polisi Tanzania Abas Abas,
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MSHAMBULIAJI hatari wa Tanzania Prisons ya Jijini Mbeya inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, lsmail Mgunda Maarufu ‘Suma’ jana ameng’ara kwenye fainali ya The Gunners Ndondo Cup kati ya Sarange Fc inayomilikiwa na wapiga debe wa Stend ya Msamvu akiwemo bondia Karim Mandonga na Wakushi Fc ya Mitaa ya Manzese Kata ya Mafiga Mkoani hapa.
Fainali hiyo iliyopigwa jana jioni uwanja wa Saba saba Morogoro, imevunjika dakika ya 78 baada ya Sarange kufunga bao la kusawazisha ambalo lilikataliwa na Mwamuzi James Andrew.
Hali hiyo iliwachukiza mashabiki wa Saranga ambao kipindi cha kwanza dakika 31 walisawazisha bao hilo lakini mshika kipendera Mwarabu Mumba alinyoosha kibendera akidai mfunga wa bao hilo Hasan Mkota Messi wa Chamwino alikuwa eneo la kuotea kabla ya kufunga.
Wapiga debe hao walioongozwa tajiri Abdallah Al- Saed akiwakilisha kampuni yao ya mabasi ya Al- Saed walinung’unika nje ya uwanja bao bao lao kukataliwa.
Walipambana na dakika ya 78 walifanikiwa kupachia bao ambalo pia lilikataliwa na Mwamuzi James Adrew hivyo baadhi ya mashabiki wa Sarange uzalendo uliwashinda wakaamua kuingia uwanjani na kumvamia refa huyo wa daraja la kwanza.
Refa huo alipoona kundi hilo la mashabiki likitaka 'kummandonga' alitia firimbi mfukoni na kutimua mbio kama Swala hadi nje ya uwanja walipoketi Polisi na Mabaunsa waliokuwa wakilinda usalama uwanjanu hapo.
Andrew alipofika kwenye mikono salama ya Polisi alizama mfukoni akatoa filimbi na kumaliza mchezo huo. Kabla ya vulugu hizo kutokea Mshambulia wa Wakushi Fc lsman Mgunda’Suma’ ambaye kwenye gemu ya juzi kati ya Simba na Prisons Suma aliisumbua sana ngome ya Simba hasa beki mkongoma Man lnonga ambaye kwa mara ya kwana alitolewa nje na kocha Juma Mgunda ambaye badae alipoulizwa na Waandishi alisema lnonga aliumia hivyo aliamua kumtoa.
HISTORI FUPI YA SUMA.
Ismail Mgunda’Suma’ alikuwa mshambuliaji wa Burkina Faso ya Mkoani hapa iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza kwa miaka 9 mfurulizo kabla ya kushuka hadi daraja la 3.
Baada ya kuuwasha Moto na Burkina Viongozi wa Stend United ya Shinyanga wakati ikiwa ligi kuu walivutiwa na kiwango Suma wakamsajiri timu hiyo ya Shinyanga aliposhuka daraja Suma alireja nyumbani Morogoro akizitumikia timu mbali mbali za madaraja la chini ikiwemo Moro Worrios iliyoshiriki michuano ya Ndodo Cup iliyotamatika hivi karibu jijini Dar ambapo Suma aliuwasha moto mkali kwenye michuano hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media.
Baada ya michuano hiyo kutamatika tumesikia Suma kajiunga na Prisons ya Mbeya hivyo tunahisi Viongozi wa Prisons walivutiwa na kiwango cha Suma kwenye michuano hiyo na kuamua kumsajiri. Gemu ya Simba na Prisons ilipotamatika wachezaji wa Prison walipewa mapunzika mafupi ambapo Suma na Jamal Masenga wanaoitumika timu hiyo ya wajelajela waliamua kureja nyumbani Morogoro.
Mwandishi wa Mtandao huu jana alimshuhudia Jamal Masenga uwanja wa saba saba akiwa jukwaani akishuhudia fainali hiyo.
Masenga anayeishi Msamvu eneo la Ndege wengi naye alijiunga na Prisons Msimu huu akitokea Mtibwa Sugar.
Jamal ambaye anatoka familia ya Mpira ambapo baba yake Mkubwa Hamad Masenga alikuwa kiunga hatari wa Reli ya Morogoro na baba yake mzazi ldd Masenga alikuwa kipa namba moja wa Burkinafaso huku baba yake mdogo Mbaraka Masenga alikuwa winga hatari wa Polisi Morogoro kwa sasa Polisi Tanzania.
Hivyo Jamal akiwa mdogo wazazi wake hao walimpekea kwenye taasisi ya Moro Kids ambapo baadae alipelekwa Mtibwa B kabla ya misimu miwili iliyopita kupandishwa timu ya wakubwa ya Mtibwa Sugar.
Mastaa wengine walishuhudiwa na Mtandao huu jana ni Abas Abas anayekipiga Polisi Tanzania na Jerry Santo aliyewahi kutamba na timu mbali mbali za ligi kuu.
No comments:
Post a Comment