Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, September 15, 2022

EXCLUSIVE INAUMA SANA. NYUMBA ALIOPANGA MTUMISHI WA MUNGU YATEKETEA KWA MOTO AKIWA IBADANI KANISANI.

Katekista Mpanda akihojiwa na Mtandao huu juzi jumanne kwenye nyumba hiyo iliyoteketea kwa moto ambayo kwa sasa imebomoka kabisa kama inavyoonekana Pichani
...Nyumba hiyo ikiteketea kwa moto Jumapili saa 12 jion

 

 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

 INASIGITISHA SANA.

 Juzi Mtandao Pendwa wa Shekidele Uliripoti habari ya nyumba nyingine kuteketea kwa moto Mtaa wa Makaburi C kata ya Mji Mpya Mkoani hapa na kuahidi kuposti habari ‘Exclusive’ ya tukio hilo.

 

Mtandao huu unakupasha habari ya chini ya kapeti kwamba miongoni mwa wapangaji wa nyumba hiyo ni Mtumishi wa Mungu Katekista wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro anayeongoza Kigango cha Mtakatifu Telesia wa Mtoto wa Yesu kilichopo Kata ya Mji Mpya Sevelini Mpanda.

 

Imeelezwa kwamba wakati nyumba hiyo ikiteketea kwa moto Jumapili Majira ya saa 12 jioni Katekista Mpanda ambaye pia ni kiongozi Mkuu wa Kwaya zote za Parokia ya Morogoro kwa maana ya shirikisho la Kwaya alikuwa  lbada kanisani.

 

 Katekista huyo pia ni Mpiga Kinanda Mkuu wa Kanisa Kuu la Mt. Patrick vile vile ni Kwaya Master wa Kwaya ya  Mtakatifu Francis ya Kanisa kuu la Mt Patrick.

 

Hivyo wakati nyumba hiyo ikiteketea kwa moto yeye na familia yake walikuwa kwenye lbada kanisa kuu la Mt Patrick, hivyo hawakufanikiwa kuokoa hata kijiko kwenye chumba chao ambacho walikifunga na kwenda kumuabudu Mungu kanisania.

 

Mara baada ya kunyaka habari hiyo nzito ambayo huwezi kuopata popote zaidi ya Mtandao pendwa wa Shekidele, Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Katekista huyo kwa takribani siku mbili na kufanikiwa kumpata juzi jumanne Septemba 13 ambapo alithibitisha Vitu vyake vyote kuteketea kwa Moto wakati akiwa kanisani.

 

”Tunapaswa tumshukuru Mungu kwa kila jambo ni kweli vitu vyangu vyote vimeteketea kwa Moto nikiwa kanisani mimi na familia yangu, kwa sasa tumebani na  nguo tulizovaa pekee”alisema Katekista huyo.

 

Alipotakiwa kuzungumzia mazingia alivyopata taarifa za tukio hilo pia kujua  kwa sasa inaishi wapi? Mtumishi huyo wa Mungu alisema.

 

”Kama kawaida kwa kuheshimu lbada huwa tunazima simu kanisani hivyo baada ya lbada kwisha majira ya saa 12 na nusu jioni nilipowasha simu nimeona meseji zinaingia wakati naendelea kuzisoma nikapigiwa simu kwamba nyumba yetu inaungua nikaja hapa nyumbani na kushuhudia nyumba yote imeungua na kubomoka kama unavyoiona sikutoa hata kijiko Shekidele.

 

“Kuhusu swali lako la Pili kwa sasa nimehifadhiwa na msamalia mwema Luis Joseph Mtandika pale mtaa wa pili, namshukuru sana huyu jamaa bila yeye nahisi ningeumbuka hapa mjini”alisema mtumishi huyo wa Mungu.

 

Alipoulizwa kwamba Kanisa halikumsaidia kwenye janga hilo alijibu, “Mpaka sasa kanisa bado halijanisaidia huenda bado wanajipanga kufanya hivyo, kuhusu wenzangu wa Kigango huwa tunakutana kila siku za Jumamosi hivyo namini hao tukikutana kesho kutwa jumamosi wanaweza kunipa pole ”alisema Katekista Mpanda kwa sauti ya Upole.

 

Kwa yoyote atakayeguswa na majanga yaliyomkuta mtumishi huyo wa Mungu awasiliane naye kwa namba yake ya simu 0784 36 16 53.

 

Mahojiono na Katekista huyo pia yamerekodiwa hivyo Clip video ya mahojiano hayo Mwanzo mwisho yataruka hewani hivi Punde YouTube’Shekidele Tv Online’

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...