Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, September 18, 2022

MUNGU ANACHUKIA WATU KUACHANA. UJUMBE WETU LEO JUMAPILI UNATOKA


 Pikipiki ya Mwandishi wa Mtandao huu ukiwa Mlima Ng’aro barabara kuu ya Bigwa -Kisaki ambapo ukishuka Mlima huo unaingia Kijiji hicho cha Kiloka

MALAKI 2-15-16.

 

”Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi,ambaye alikuwa na ufahamu kidogo.Au  je kuna mtu mmoja atafutaye mzao  mwema kumcha Mungu?kwa hiyo jihadharini  roho zenu mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.

 

Maana mimi nachukia kuachana  asema Bwana Mungu wa lsraeli naye ajifunikizaye nguo yake  kwa udhalimu na mchukia asema Bwana wa Mjeshi,basi jihadharini roho zenu msije mkatenda kwa hiana”

 

   UCHAMBUZI WA NENO LA MUNGU.

 

Kwa sasa ukifungua Redio, Tv au ukiingia kwenye Mitandao ya Kijamii utakutana na Vilio vya mapenzi watu kuachana sababu kubwa ikiwa usaliti, mbaya zaidi kwa sasa habari nyingi kwenye vyombo hivyo vya habari ni mauaji yanayosababishwa na wivu wa Mapenzi.

 

Kwenye ujumbe huo wa Mungu Mstari wa 15 Mungu anatoa agizo kali kwamba mtu awaye yote asimtende mke wa Ujana wake mambo ya hiana.

 

 Mungu kataja Vijana kwa sababu ndio wenye tamaa wakikosa uvumilivu,  ndoa nyingi zinazovunjika kwa sasa kundi kubwa ni za Vijana.

 

lfahamike Mungu kasema awaye yote asimtende mwenzi wake  hivyo na nyinyi wake msiwatende waume zenu kwa hiana.

 

Muda huu niko njiani naelekea Kijiji cha Temete A Kata ya Kiloka Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki linaloongozwa na Hamis Tale Tale Maarufu Babu Tale ambaye pia ni Meneja wa Msanii Maarufu Afrika wa Muziki wa Kizazi Kipya Mtanzania Nassib Abdul Diamond Platnums.’

 

Juzi ljumaa  Septemba 16 usiku mnene kwenye Kijiji hicho kilichopo takribani kilometa 25 kutoka Morogoro Mjini. kumetoka mauaji mwanaume mmoja anadai kumuua mwanaume mwenzake akimtuhumua kutembea na Mwanamke aliyezaa naye.

 

Asubuhi wakati natoka nyumbani kwenye redio nilisikia Muvi inayozungumzia watu kupelekana Polisi kisia usaliti, baada ya Muvi hiyo kutamatika Mtangazaji wa redio hiyo kaweka wimbo wa Msanii kutoka Kenya unaokwenda kwa jina la Stela Uwanja wa ndege.

 

Hivyo kwa matukio hayo nimeona iko haja kutafuta ujumbe wa neno la Mungu unaokemea usaliti lengo ni lile lile kukumbushana na kuikumbusha nafasi yangu

 

Kwa leo Mtumishi wenu naishia hapa Mungu akipenda tukutane Jumapili ijayo kwa somo lingine.

                

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...