Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, September 19, 2022

A-Z UNDANI WA MAUAJI YA BODA BODA ALIYEUWAWA CHUMBANI KWA MPENZI WAKE KIJIJI CHA KIL OKA MORO.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro akizungumza na Waandishi wa habari akiwasilisha matukio mbali mbali likiwemo hilo la mauaji ya Kiloka
Marehem Rashid Said Maharagande enzi za uhai wake.
 


               Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

NAJUA taarifa za tukio la Mauaji yaliyotokea Kijiji cha Kiloka Mkoa hapa, yanayohusishwa na Wivu wa mapenzi umezipata kupitia vyombo mbali mbali vya habari, Mtandao huu umetinga maeneo ya tukio na kukusanya habari za chini ya kapeti za tukio.

 

Baada ya kutokea kwa tukio hilo Septemba 16 Majira ya saa 8 usiku ndani ya  chumba kinachomilikiwa na Mwana dada Salapita Thomas[21]kilichopo Kitongoji cha Temekero ‘A’ Kata ya Kiloka Tarafa ya Mkuyuni Jimbo la Morogoro Kusini linaloongozwa na Mbunge Hamis Tale Tale ambaye Pia ni Meneja Mkuu wa Msanii nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya barani Afrika Mtanzania Nassib Abdul

’Diamond Platnums.’

Mwandishi wa habari hizi alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendokasi hadi  eneo la tukio umbali wa takribani kilomita 25 kutoka Morogoro Mjini  na kuchimba undani wa mauaji hayo A-Z.

 

Awari Mwandishi wa habari hizi alizungumza na Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Hamis Abdallah ambaye alipotakiwa kueleza tukio hilo alikuwa na haya ya kusema.

 

”Huyu mwanamke alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Richard Chanzila kwenye mahusiano yao wamejaliwa kuzaa mtoto lakini baadae walitofautiana wakaachana Salapita kamua kupanga chumba na kuanza maisha Mapya ya upweke.

 

Siku ya tukio hapa Kijijini kulikuwa na sherehe kikapigwa kigodoro usiku wanakijiji  tulikusanyika akiwemo Salapita na Richard, baada ya sherehe kwisha watu tulitawanyika akiwemo Salapita.

 

 Nasikia baada ya kuachana na mzazi mwenzake Salapina alipata bwana mwingine anayeishi Mjini”alisema shuhuda huyo na kuongeza kudadavua.

 

Kwenye Kigodoro hicho Salapina alikuwa na huyo jamaa yake wakisakata Rhumba, baada ya kumuona mzazi mwenzake na mwanaume huyo Richard akajawa na wivu na kuamua kuwafuatilia hatu kwa hatu Salapina na Mpenzi wake huyo Mpya ambaye hapa kijiji hatumfahamu.

 

Baada ya sherehe kwisha Salapina alipanda kwenye boda boda iliyokuwa ikiendeshwa na mpenzi wake huyo Mpya kutoka Town wakaelekea kulala kwenye chumba cha Salapina na sikia huku nyuma Richard kakusanya marafiki zake wakatika kwenye chumba hicho usiku huo huo na kumuua jamaa huyo huku Salapina akifanikiwa kukimbia akiwa uchi wa Mnyama”alimalizia kusema shuhuda huyo. Shuhuda mwingine Asha Juma alisema

 ” Kweli mapenzi matama Jamaa kila wiki alikuwa akichoma mafuta kutoka Mjini kuja Kiloka kulala kwenye chumba cha Mpenzi wake mimi niwaase wanaume wasipende kwenda kilala kwa kwenye nyumba vinavyomilikiwa na wanawake sisi wanawake dhama hizi wengi wetu sio waaminifu tunakuwa na wanaume zaidi ya watatu kila mmoja mwisho wa mwezi unamdai kodi ya chumba sasa ikitokea siku wakifumaniana ndani yanatokea majanga kama haya”alisema Mwanake huyo anayeonekna kujistili vizuri akiwa na hofu ya Mungu.

 

Diwani wa Kata ya Kiloka Mh Jamila Taji na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Temekero A Banzi Bonzo wote walithibitisha kutokea kwa mauaji hao kwenye eneo lao.

 

”Tukio hilo limetokea usiku septemba 16 baada ya kumalizika kwa Kigodoro huku sababu ya mauaji hayo ikiwa ni wivu wa Kimapenzi natoa wito kwa wanawake kuacha tabia ya kuchanganya wanaume katika mahusiano”alisema Diwani huyo mwenye asili ya Kiarabu.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu akizungumza na Waandishi wa habari  juzi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

 Alisema tukio hilo limetokea Septemba 16  Majira ya saa 8 usiku  Kitongoji cha Temekero Kijiji cha Kiloka Tarafa ya Mkuyuni Wilaya ya Morogoro. 

Musilim alisema Mauaji hayo yanahusishwa na Wivu wa Kimapenzi ambapo Richard Chanzila[23] Mkazi wa Kitongoji cha Maembe  Kijiji cha Kiloka ndiye anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo nyumbani kwa Salapina Thomas[21]ambaye ni mzazi mwenzie.

 

Big bosi huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro aliendelea kusema mtuhumiwa  anadai kumuua Rashid Maharagande[[20] Mkazi wa Kata ya Sultan Area Morogoro Mjini kwa kitu chenye ncha kali chumbani kwa mwanamke huyo kisha Muuaji huyo kutokomea kusiko julikana.

 

Kamanda huyo  amesema wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa  ili sheria ichukue mkondo wake huku akithibitisha kumshikilia Mwanamke Salapina akihusishwa na mauaji hayo.

 

 Marehema Maharagande aliyezikwa juzi Septemba 17 kwenye makaburi ya familia yao Kididimo Jirani na Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine’SUA’ alikuwa dereva wa  boda boda Morogoro Mjini.

 

 Baada ya kutoka Kiloka Jana Mwandishi wa Mtandao huu alitinga nyumbani kwa Marehemu Sultan Area ambapo baba mzazi wa marehemu Mzee Said Maharagande amefunguka mazito kuhusiana na kifo hicho cha Mpendwa Mtoto wake.

 

Taarifa hiyo itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote. 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...