Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, September 2, 2022

MBIO KALI ZA MMOJA WA WASHIRIKI WA MOROGORO SELOUS MARATHON ZA SABABISHA AJARI.





 


 

        Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

HIVI karibu mkoa wa Morogoro ulikuwa Mwenyeji wa mashindano ya mbio ndefu na fupi zilizoshirikisha washiriki kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania.

 

Mbio hizo zilizoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Fatma Mwasa zilizofanyika Agost 20 kwenye viwanja vya gofu,kuzunguka mitaa mbali mbali ya Mji wa Morogoro na kurejea eneo hilo la Gofu.

 

Wakiwa huko Mitaani Mmoja wawashiriki wa mashindano hayo aliyefahamika kw ajina Moja la lrene kutoka kwenye moja wa Jogging za Mkoa wa Morogoro mbio zake ziliwavutia watu wengi wakiwemo madereva wa Bajaj ambapo mmoja wamadereva hao wa Bajaj inayofanya safari zake kutoka Mjini eneo le Juwata kuelekea Bingwa alijikuta akisababisha ajari kwa kumgonga Mwendesha baiskri aliyekuwa mbele yake wakati akiwa bize kumshangaa Mwanariadha huyo wa kike aliyejaliwa kuwa na Mwili mkubwa.

 

Hata hivyo kwa vile dereva huyo wa Bajaj alikuwa mwenye mdogo hakuweza kumjeruhi dereva huyo wa baiskeli aliyekuwa mbele yake,hivyo waliyazungumza yakaisha kiro safi na kila mmoja akaendelea na safari yake huku mwana dada huyo Mrembo  akiendelea kutimua mbio huku akiangua kicheko.

 

Watu wengine waliovutiw ana mbio za Mwanariadha huyo ni askari wa kikosi cha usalama barabarani ambaye naye alionekana kumshangaa Mwanariadha huyo.

 

Mwandishi wa Mtandao huu anayetumia kamera za kisasa zenye uwezo wa kutipiga picha matukio 5 kwa sekunde 5 alinaswa matukio hayo mubasha kama yanavyoonekana Pichani

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...