Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, September 3, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU LEO JUMAPILI LINATOKA.


  Mtumishi wako wa Mtandao huu akiitafakari dunia hii iliyojaa tabu na mateso Mengi


 

                YEREMIA 18.6-10

 

”Ee nyumba ya lsrael je siwezi mimi kuwatendea ninyi  vile vile kama Mfinyanzi huyu aliyotenda?

 

.Asema Bwana, angalieni kama  udongo ulivyo katika mkono wa Mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika Mkono wangu, Ee nyumba ya lsraeli.

 

Wakati Wo wote nitakapotoa habari za taifa  na habari za ufalme kuung’oa na kuuvunja na kuuangamiza.

 

lkiwa  taifa lile nililolitaja litageuka na kuacha maovu  yake nitaghairi nisitende mabaya yake niliyoazimia kuyatenda.

 

 Na wakati Wo wote nitakapo toa habari  za taifa na habari za Ufalme kujenga na kuupanda.

 

Ikiwa watatenda Maovu mbele za Macho yangu,wasiitii sauti yangu, basi nitaghairi nisitende Mema yake niliyoazimia kuyatenda”

 

 UCHAMBUZI WA NENO HILI LA MUNGU.

 

Mpendwa Mwana wa Mungu taifa lililotajwa hapo ni mimi na wewe Mungu anatueleza kwamba tukizisikiliza habari zake na tukayaacha maovu ataghairi kutupa adhabu tunazostahiri.

 

Lakini akatuasa tena akisema tukifanya maovu tena mbele ya macho yake ataghairi pia kutupa yale mema aliyoazimia kututendea.

 

Kwa kizazi hiki baadhi ya watu tunasoma habari za Mungu zinazotukataza kuacha mabaya na kutuelekeza kufanya mema lakini tumeifanya mioyoyetu kuwa migumu tukidanganywa na kiburi cha uzima.

 

Habari hizo za Mungu tunasisikia sana kupitia kwa viongozi wetu wa dini zote, vile vile habari hizo hizo za Mungu huwa tunazisikia kupitia vyombo vya habari Radio,Tv na Mitandao ya Kijamii ukiwemo Mtandao Pendwa wa Shekidele ambao kila jumapili huweka kando habari zote za kidunia na kuripoti habari za Mungu.

Utakuta mtu analalamika  kila siku kwamba kila anachofanya hafanikiwa,nakusihi ujitathmin huenda umemchukiza Mungu hivyo ameghairi kukupa mema yako, kwa sababu bado unapunzi na badilika ltii sauti ya Mungu naye akupa mema yako, maisha bora unayoyahitaji, mke au mume bora unayemtamani.

 

 Hivyo sidhani kama kuna mtu yoyote kesho mbele ya huku ya  Mungu atakuwa na utetezi  kwamba hajazisikia habari hizo za Mungu.

 

 Ahadi yangu kwako Mpendwa msoma wa habari hii Mungu akiendelea kunipa zawadi ya Uhai na zawadi ya Afya nyema kila jumapili nitaendelea kuripoti habari hizo za Mungu kwa lengo la kukukumbusha na kuikumbusha nafsi yangu  kwani namini na mimi ni miongoni mwa wakosefu.

 

Mwenye masikio na asikie asiye na masikia….], Kwa leo naishia hapa Mungu akipendwa tukutane jumapili ijayo kwa some lingine Mungu akubariki sana huku akikufanyia wepesi wa kuacha dhambi.

 


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...