Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, September 20, 2022

MAUAJI YA BODA BODA KWENYE TUKIO LA FUMANIZI BABA AFUNGUKA MAZITO.

Said Maharagande baba mzazi wa Marehemu akizungumza na Matndao huu
Marehemu Rashid Said Maharagande enzi la Uahi wake
Nyumbani wa Marehemu akiwemo baba mdogo wa Marehemu Kafale Maharagande mwenye Suliali Nyeusi

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro akitoa taarifa za matukio mbali mbali kwa Waandishi wa habari likiwemo tukio la Mauaji hayo


         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Jana Mtandao Pendwa wa Shekidele uliripoti A-Z tukio la Mauaji ya dereva wa boda boda Rashid Said Maharagande[20]Pichani mwenye begi mgongoni enzi la Uhai wake

 

Baada ya kutoka eneo la tukio Kitongoji cha Temekero ‘A’Kata ya Kiloka Tarafa ya Mkuyuni Wilaya ya Morogoro,Mwandishi wa habari hizi alitinga nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Sultan Area katikati ya Mji wa Morogoro na kufanikiwa kuzungumza na Said Maharagande ambaye ni baba mzazi wa marehemu na baba mdogo wa Marehemu Kafale Maharagande ambapo kwa pamoja wamefunguka mazito kuhusiana na kifo hicho cha ghafla cha mtoto wao.

 

Katika mahojiano hayo awari Said Maharagande alitakiwa kueleza kwa ufupi historia fupi ya marehemu mtoto wake.

 “kama unavyomuona mwanangu bado mdogo hajao wala hana mtoto, alipomaliza shule nilimtafutia Pikipiki akawa anafanya kazi ya boda boda akijitafutia riziki alikuwa akipack boda boda yake kijiwe cha Rock Garden jirani na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

 

Siku ya tukio Mwanangu hakurejea nyumbani tukamtafuta kwenye simu hakupatikana kulipokucha tukaanza kumtafuta ndipo tulipopata taarifa kwamba ameuwawa Kiloka, huyu baba yake mdogo na ndugu wengine walikwenda eneo la tukio na kumkuta Mpendwa mtoto wangu Rashid ameuwawa kikatili.

 

Kwa kushilikiana na Polisi waliuchukua Mwili na kuleta Mjini ambapo jana Septemba 17 tumemzika  kwenye makaburi ya Kididimo SUA, Mwanangu amezimika kama mshumaa kifo chake cha kikatili kimeniuma sana sina jinsi namuachia Mungu na Jeshi la Polisi wafanya kazi yao” alisema Mzee huyo Pichani mwenye Kanzu na Bagharashia.

 

Kwa upande wake Kafale Maharagande baba mdogo wa Marehemu Pichani mwenye Suluali nyeusi alipotakiwa kueleze tukio hilo alisema “Shekidele inauma sana nilifika eneo la tukio Kilosa nimekuta mwili wa Mwanangu ukiwa uchi wa mnyama umetupwa kichakani mita kama mia kutoka kwenye chumba cha Mwanamke aliyekuwa naye huku shingoni ukiwa na jereha.

 

Mimi na Polisi tulienda  kwenye chumba hicho tukakuta kimefungwa na kufuli Mwanamke huyo akamuliwa akifungue tulipoingia ndani tukakuta damu kibao kitandani huku zile damu za sakafuni zikionekana kupigwa deki.

 

 lnaonekana baada ya Rashid kuwawa kwenye chumbani hicho na watuhumiwa hao kukimbia na kuuacha mwili ndani ya chumba hicho,huenda Mwanamke huyo kwa kushirikiana na ndugu zake waliutoa mwili wa Rashid usiku huo huo na kwenda kutupa kichakani kwa lengo la kupoteza ishahidi kwenye chumba hicho.

 

 Tulipomhoji Mwanamke huyo eneo la tukio alisema akiwa amelala na Rashid, Mzazi mwenzake aliingia ndani usiku huo akiwa na kundi la wenzake wakawaamulu kuvua nguo na Mzazi mwenzake huyo akawaambia leo na waua wote wawili.

 

Mwanamke huyo akaendelea kusema alipoona Rashid anapigwa na silaha mbali mbali zikiwemo zenye ncha kali  kamua kukimbia akiwa uchi wa mnyama akielekea kwa Mama yake anayeishi eneo hilo.

 

Kama familia tunashangaa kama huyo Mwanamke alikua bado anamahusiano na huyo Mzazi mwenzake kwa nini amemficha mtoto wetu na kumpa uhuru kwa kwenda kulala nyumbani kwake?”. Alisema Mzazi huyo kwa uchungu

 

Alipoulizwa ilipo Pikipiki ya Marehemu, Kafale alisema “Tulipofika eneo la tukio Pikipiki hiyo tumeitafuta bila mafanikio huenda watuhumiwa hao wameondoka hayo”alisema Kafale Maharagande ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Wilaya ya Morogoro.

 Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilim amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

 

 Musilim alisema  Mtuhuniwa wa mauaji hayo  Richard Chanzila[23] baada ya tukio hilo alikimbia na kwamba Jeshi hilo linamsaka kwa udi na uvumba ili sheria uchukue Mkonde wake.

 

 Kamanda huyo alisema kwa sasa wanaendelea kumshikilia Salapina Thomas[21] Mwanamke anayedaiwa Kuzaa na Chanzila huku akingia kwenye mahusiano Mapya nakumkabilisha nyumbani kwake Mpenzi wake Mpya Marehemu Rashid Maharagande.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...