Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, September 12, 2022

MAJANGA. NYUMBA NYINGINE YA TEKETEA KWA MOTO KATA YA MJI MPYA MOROGORO.

Maafande wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji wakiendelea kuuzima Moto huo
Maafande wa Zima Moto wakizama ndani kuzima Moto huo

Polisi wenye silaha wakiwadhibiti wananachi wasisogee eneo la Moto

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Makburi C Abdallah Ally Mkawa akihojiwa na Mtandao huu jana eneo la tukio
Dishi ya Azam iliyokuwa ikimilikiwa na mmoja wawapangaji imenusurika
Vigogo wa CCM Kata ya Mji Mpya wakiongozwa na katibu Mwenyezi kata ya  CCM Kata ya Mji Mpya Seleman Kasanga[kulia aliyeshika kiuno wakishuhudia nyumba hiyo ikitekekea kwa Moto
Nguzo ya Umeme ikiwa jirani kabisa na nyumba hiyo inayoteketea kwa Moto


 

 

 

                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

NYUMBA nyingine imeteketea kwa moto Mtaa wa Makaburi C kata ya Mji Mpya Mkoani Morogoro, baada ya nyumba nyingine kuteketea kwa moto  Mtaa wa Makaburi B kata hiyo miezi 2 iliyopita.

 

Tukio hilo la moto ambalo halikuua wala kujeruhi binadamu yoyote ingawa limeteketeza mali za wapangaji wote  limetokea  jana majira ya saa 12 jioni.

 

Mara baada ya kutokea kwa moto huo ambalo chanzo chake mpaka sasa  hakijajulikana, Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Jeshi la Polisi, Viongozi wa Serikali ya Mtaa pamoja na Mwandishi wa habari hizi kwa pamoja waliwahi eneo la tukio kila upande ukiwajibika kwa nafasi yake.

Pongezi za pekee ziwafikie Jeshi la Zima Moto kwa kuwahi eneo la tukio na kufanikiwa kuthibiti Moto huo usisambaye kwenye nyumba nyingine zilizopo jirani na nyumbani hiyo ambazo zote zilikuwa zimeunganishwa Nishati ya Umeme ikiwemo baa Maarufu ya Night Club ya Vatican inayojaza watu wengi siku za Wiki End ikiwemo siku hiyo tukio jana Jumapili.

 

Kwa upande wa Jeshi la Polisi nao walifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti watu wasisogee eneo la Moto isije kutokea kama yale yaliyotokea kwenye Mlipuko wa Lori la Mafuta uliotokea eneo la Msamvu Agost 10 2019 Majira ya saa 12 asubuhi ambapo zaidi ya watu 95 waliosogea eneo la tukio kwa lengo la kugema Mafuta walifariki dunia na wengi kujeruhiwa.

 

Kwa uapnde wa Mwandishi wa habari hizi yeye alisogea eneo la tukio na kufanyakazi yake ya kupiga Picha matukio yote ya Moto huo sambamba na kuwahoji Viongozi wa serikali ya Mtaa huo na baadhi ya wapangaji wa nyumba hiyo.

 

Akihojiwa na Mtandao huu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makaburi C Abdallah Ally Mkawa,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye Mtaa wake.

 

”Nikijubu Maswali yako nyumba hii ni namba 18 kitalu namba 10 inamilikiwa na Mzee Zuberi Said ambapo msimamizi Mkuu kwa sasa ni mwanae Jumanne Zuberi.

 

Kuhusu chanzo cha Moto bado hatujafahamu na hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa ingawa mali zao zinaendelea kuteketea kwa moto kama unavyoshuhudia ndugu Mwandishi”alisema Mwenyekiti huyo.

 

 Kwenye tukio hilo la Moto Mwandishi wa Mtandao huu amenasa habari ya chini ya kapeti kuhusiana na Moto huo, habari hiyo itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 Ikumbukwe takribani Miezi 2 iliyopita nyumba  ya Kigogo wa CCM Kata ya Mji Mpya Bi Nasma Ndehele  iliyopo mtaa wa Makaburi B unaotengana na Mtaa huo wa Makaburi C pia iliteketea kwa Moto.

                   

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...