Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, September 10, 2022

KUMBUKIZI. GAUNI LAMTO NISHAI IRENE UWOYA MKUMBINI



 Baada ya kufanikiwa kufika jukwaani salama Uwoya akiwa na karatasi yake yenye majina ya Top 5 akiliweka sawa gauni hilo

.
  Na V.A.R Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
Miaka kadhaa iliyopita Msanii nyota wa Sinema za kibongo’Bongo Movi’Irene Uwoya, aliteuliwa kuwa Mmoja wa Majaji wa Shindano la Miss Morogoro 2019,lililofanyika katika hotel ya Kitalii ya Morogoro Maarufu Morogoro Hotel. 
 
Katika shindano hilo moja ya matukio yaliyonaswa na Mwandishi wa habari hizi ni gauni la pesa ndefu lenye Mpasu Mkubwa kama Mto wa Morogoro kumtoa nishai Super Star Uwoya mwenye jina lake Mjini.
 
Kipembe kilianzia pale Irene Uwoya alipotakiwakupanda jukwaani kutangaza warimbwete watano waliofanikiwa kutinga [Top 5]ambapo alitumia takribani dakika 10 kupanda ngazi 4 za jukwaa hilo.
 
Alipofika ngazi ya 2 viatu vyake virefu vimenasa kwenye kauni kayumba alipotaka kuanguka Ma Mc wawili wa Shughuri hiyo waliwahi kumdaka na kumshika mkono huku wakimsaidia kumalizia ngazi 2 zilizobaki. 
 
Paparazi wa Mtandao huu alikuwa bize kazini kumtwanga Mapicha Mkali huyo wa Bongo Muvie hatua kwa hatu. 
 
Mara baada ya kutangaza Top Five hiyo Uwoya alimuomba tena Mc kumsaidia kushuka ngazi hizo huku Umati mkubwa wawatu uliofurika kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumsaka Mrimbwende wa Mkoa wa Morogoro wakimkodolea macho huku wakingine wakimsengenya kwa Vazi hilo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...