Vigogo wa Polisi wakimkabidhi koti hilo Mwandishi wa habari wa Mtnadao huu kushoto
Vigogo wa Polisi na Waandishi wa habari wakipiga Picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bwalo, akiwemo Mwandishi wa Mtandao huu mwenye kofi nyeupe kati
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
UMOJA wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania’ UT.P.C’ Umetoa nguo zitakazomtambulisha Mwandishi wa habari anapokuwa kwenye majukumu yake ya kazi hasa kwenye maeneo hatarishi.
Akizungumza kwenye kikao kazi kati ya Waandishi wa habari na Vigogo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro,Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’ Nickson Mkilanya alisema wiki iliyopita alikuwa jijini Mwanza yalipo Makao Makuu ya Union Of Tanzania Press Clubs’UTPC’.
“Kwenye kikao hicho cha U.T.P.C wenye viti wote wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania tulipewa Makoti Machache tuwakabidhi Wanachama wetu wanapokuwa kwenye majukumu yao ya kazi”. alisema Mkilanya na kuongeza.
“ Baadae yatakuja mengine lakini kwa leo Makoti hayo 16 tutawakabidhi Waandishi wa habari 16 mbele yenu kama kitambulisho wanapokuwa kwenye majukumu yao ya kazi, hivyo hatutaraji kuona tena Mwandishi akinyanyaswa awapo kazini”alimalizia kusema Mwenyekiti huyo.
Miongoni mwa waandishi hao waliopata bahati ya kupewa koti hizo ni pamoja na Mwandishi wa Mtandao huu
Utamburisho huu wa Makoti pia huvaa Waandishi wa habari wanaporipoti habari kwenye vita, ambapo kufuatia utamburisho huo Wapiganaji’Wanajeshi’ wa pande zote mbili wakiona Mwandishi wa habari kavaa koti hilo lenye Maandishi ya Press hawamgusi na hilo ni agizo la Umoja wa Mataifa.
Baada ya kikao hicho Waandishi na Vigogo wa Polisi walipiga Picha ya pamoja nje ya ukumbi huo wa JKT Bwalo la Umwema.
Habari zaidi za kikao hicho zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment