Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, August 5, 2022

LIGI KUU ENGALND, ARSENAL YATUMA SALAM KALI KWA VIGOGO WA LIGI HIYO



 

 NJIWA PELEKA SALAM KWA MAN U.

PAZI la Ligi kuu ya England limefunguliwa leo majira ya saa 4 usiku kwa  Arsenal kuitandika timu ngumu ya Crystal Palace nyumbani kwao  bao 2-0.

 

. Gemu hiyo tafu imetamatika muda huu saa 6 usiku na Moja kwa moja, shabiki kindaki ndaki  wa Arsenal Shekidele ‘Mkude Simba’ a.k.a Ez Come Ez Go amewasha Lap Top  usiku huu na kuwapa matoke wale wasiobahatika kucheki gemu hiyo iliyokuwa tamu kwa muda wote wa dakika 90,.

 

.Kwa ushindi huo Chama la Wana Arsenal imekuwa timu ya kwanza kuongoza ligi hiyo pendwa duniani.wenginge watakao ongoza ligi hiyo huko mbele watafuata njia iliyochongwa na Arsenal.

 

 

Ushindi huo mnono wa washika bunduki hao wa  Jiji la Maraha la London ni salama kwa mahasimu wake wakubwa Vigogo vya ligi hiyo, Manchester United, Chelsea, Manchester City, na Liverpool.

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...